Wauza mkaa tumepokoywa leseni: Maharage yenu chemsheni kwenye Gas tu!

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,551
22,097
Vibali Vya kusafilisha mkaa vimepigwa marufuku na kufutwa vyote hususani maeneo ya ikwiriri, Mkuranga na maeneo ya jirani!

Ukiiona fuso imeingia mjini na mkaa inabidi tu huyo mwenye mkaa umpongeze!
Sasa hivi mariasili wanazunguka hadi kwenye mabanda uswahili kudai leseni ya biashara hata kama una gunia mbili!

Mkaa utaadimika; tujiandae kupika maharage kwenye jiko la mchina au Gas!
Mkaa sasa bye bye ;tunataka kurejesha ardhi ya kijani!
******************
USALAMA-2.jpg
 
Nawapongeza waliopiga marufuku ili kulinda nchi yetu isiwe janga inabidi watu kutumia alternative source ya kupikia aisee. Maliasili wahakikishe na wapasua mbao kwa kutumia machine wanakamatwa bila hivo after ten years tutakuwa jangwa na ukosefu wa mvua umeanza jitokeza.
 
Wadhibiti kabisa mkaa usiingie mjini majuzi kati hapa nimeenda kijijini kulikuwa pori lakini sasa hivi ni jangwa wakimaliza hapo wahamie kwa wachana mbao mkaa ni janga la kitaifa
 
Vizuri sana
Kwa hapa Dar Mkaa usiingie kabisa hata kuni zisiwepo watu wanunue gesi
Mkaa unaharibu sana mazingira kwani miti hukatwa
 
Nawapongeza waliopiga marufuku ili kulinda nchi yetu isiwe janga inabidi watu kutumia alternative source ya kupikia aisee. Maliasili wahakikishe na wapasua mbao kwa kutumia machine wanakamatwa bila hivo after ten years tutakuwa jangwa na ukosefu wa mvua umeanza jitokeza.
Siwapongezi kwa kuwa si kila mtanzania ana uwezo wa kununia GAS au JIKO LA MAFUTA YA TAA
 
Hivi tinapiga marufuku mkaa lkn kuna alternative gani je tutapunguza bei ya gas etc au umeme kwa wenye oven au mafuta ya taa kwa majiko ya mchina hebu tunapokuja na jambo hata kama la manufaa tuangalie side repercussion zake isije sheria ikapotea watu wakarudi pale pale kwenye mkaa
 
Wadhibiti kabisa mkaa usiingie mjini majuzi kati hapa nimeenda kijijini kulikuwa pori lakini sasa hivi ni jangwa wakimaliza hapo wahamie kwa wachana mbao mkaa ni janga la kitaifa
Mwenyewe nilienda kijijini niliumia sana watu wanapasua mbao hovyo miti yote imekatwa utafikiri hamna serikali tena waziri wa Mazingira aanzishe Sera ya upandaji miti kuanzia ngazi ya familia had kitaifa na kila RAIA lazima autunze. Mabadiliko ya tabia nchi yamezidi mno hadi kufanya mvua zipungue.
 
Siwapongezi kwa kuwa si kila mtanzania ana uwezo wa kununia GAS au JIKO LA MAFUTA YA TAA
Unataka nchi yetu iwe janga unajua mkaa gunia moja ni miti mingapi inadondoshwa. Ikipigwa marufuku watu watatumia other sources of energy kupikia.
 
Back
Top Bottom