Wauza mahindi wanaboa

uajekundu

JF-Expert Member
Jan 14, 2016
541
461
Habari zenu wajameni,

Wauza mahindi wamekua na tabia ambayo binafsi siipendi na inakera nakuniharibia appetite ya kula mahindi yao.

Utakuta mtu anachoma mahindi yanavutia hadi umate unakutoka, ukikaribia kwa ajili ya kununua na kumwambia unataka la moto ndio hapo panapokera, utakuta anaanza kuyakumbatia kwa kuyashikashika mahindi yale akijua fika hajanawa mikono na ametoka kushika hela.

Mimi kama nataka hindi in bora nilisimamie wakati linachomwa muuzaji akisha lishikashika na kulikumbatia kwa midole yake hua naondoka bila habari, wewe je?
 
Unawaambia wawe wanaacha ile sehemu ya nyuma,cha kushikia kwa ustaarabu na usafi kwa wateja, pia asiruhusu kila MTU ashike mahindi waangalie kwa macho tu
 
Si umetaka wa moto sasa atajuaje umoto uliopo kwenye muhindi

Kali ni kwa wale wanaotembeza karanga je hawaendagi msalani na wakienda kapu au ungo wa karanga wanamuachia nani(boonge la vitamini)
 
Mwingine anakuna pumbu akimaliza anashika shika hindi kwenye moto,basi tu
 
Shyeeeh...!!! uwe unawaachia thermos wakikuchomea wanakuhifadhia usisahau pia ndimu na mvichu.
 
Utaishi kwa tabu zana tanzania......ila ndio ushazaliwa na uzarendo ni kuridhika na hal alisi uzungu/usaf wengi hatuujui.
 
Habari zenu wajameni, wauza mahindi wamekua na tabia ambayo binafsi siipendi na inakera nankuniharibia appetite ya kula mahindi yao. Utakuta MTU anachoma mahindi yanavutia hadi umate unakutoka, ukikaribia kwaajili ya kununua na kumwambia unataka LA moto ndio hapo panapokera,utakuta anaanza kuyakumbatia kwa kuyashikashika mahindi yale akijua fika hajanawa mikono na ametoka kushika hela...Mimi kama nataka Hindi in bora nilisimamie wkt linachomwa...muuzaji akisha lishikashika na kulikumbatia kwa midole take hua naondoka bila habari.we we je?
....Nunua mabichi 2 ukachome mwenyewe home kwa raha zako...
 
Mahindi haya kipindi cha mvua yanakuaga matamu balaa, yani hata huwezi kulalamika kama hiviii, hizi zote shibee tuu
 
Habari zenu wajameni,

Wauza mahindi wamekua na tabia ambayo binafsi siipendi na inakera nakuniharibia appetite ya kula mahindi yao.

Utakuta mtu anachoma mahindi yanavutia hadi umate unakutoka, ukikaribia kwa ajili ya kununua na kumwambia unataka la moto ndio hapo panapokera, utakuta anaanza kuyakumbatia kwa kuyashikashika mahindi yale akijua fika hajanawa mikono na ametoka kushika hela.

Mimi kama nataka hindi in bora nilisimamie wakati linachomwa muuzaji akisha lishikashika na kulikumbatia kwa midole yake hua naondoka bila habari, wewe je?
yani wewe hii post ulivyoileta ni kama umeichukua kichwani kwangu kabisa.
pesa ni chafu sana zinapita kwenye mikono mingi sana, na kitu kingine kichafu sasa hivi ni simu.
simu hasa za kupapasa ni chafu sana.
mimi sili mahindi ya kuchoma njiani wala juice ya miwa sinywi. labda niridhike na mazingira
 
Haya sio ya hadhi yako mkuu tuachie sie wa uswazi wenunua mabichi ukayachomee kwenye jiko lako la gas au la umeme
 
Back
Top Bottom