Hapa vijana lawama zinawaepuka kwa kuwa hawa wake na waume za watu hutumia ubabe,fedha na uzoefu wa kimaisha kuwarubuni hawa vijana.Hivyo wanajikuta wanafanya bila ridhaa yao!
Kabla sijakupa muongoza wa mada yako, nikujibu hii hoja kuwa hakuna mtu mzima anayejikuta amefanya umalaya bila ridhaa yake. Ni ukosefu wa uwepo wa Mungu katika maisha yetu ndio unatufanya tushawishike kufanya dhambi.
Fuatilia hekima hii
Mwanagu, shika maagizo ya baba yako,
wala usiache sheria ya mama yako.
Yafunge hayo katika moyo wako daima,
jivike hayo shingoni mwako.
Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda,
na uamkapo yatazungumza nawe.
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru,
na maonyo ya kumwadilisha mtu na njia ya uzima.
Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate,
na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.
Usiutamani uzuri wake moyoni mwako,
wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.
Maana kwa malaya, mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate,
na kahaba humuwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani.
Je mtu aweza kutia moto kifuani pake,
na nguo zake zisiteketee?
Je mtu anaweza kukanyaga makaa ya moto,
na nyayo zake zisiungue?
Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake,
kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
Watu hawamdharau mwivi,
akiiba na kusihbisha, iwapo aona njaa
lakini akipatikana atalipa mara saba,
atatoa mali yote ya nyumba yake.
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa,
afanya jambp litakalomwangamiza nafsi yake.
Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima,
wala fedheha yake haitafutika;
maana wivu ni ghadhabu ya mtu,
wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi;
hatakubali ukombozi uwao wote,
wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.
Mithali 6:20-35
Mkuu, huwezi kukwepa lawama kwa kuwa ulisikiliza maneno ya Mwanamke. Wewe mwanaume uliumbwa, ukapewa ufahamu zaidi ya mwanamke, sasa iweje leo usilaumiwe kwa kuwa eti ulishawishiwa na mwanamke?!
Hapo kwenye Mithali 6:29, unaambiwa kila amgusaye mwanamke malaya (anayemsaliti mume wake), naye ana hatia. Kukosa kwako uadilifu, si kosa la mtu mwingine ndio maana Hekima anatuambia ''shika maagizo ya baba yako, wala usiache sheria ya mama yako''.
Eva alipompotosha Adama akavunja agano na Mungu, Mungu hakumuadhibu Eva peke yake, aliwaadhibu wote. Adam alijitetea kuwa mwanamke uliyenipa ndiye aliyenipotosha, lkn je, maagizo ya Mungu na maneno ya Eva yepi yalipaswa kufuatwa? Kwa hiyo utaona kuwa hakuna excuse kwa dhambi utakayofanya na kusingizia ulishwawishiwa.
Jihadhari na mienendo ya mwanamke, kwani ukamilifu wake u mashakani tangu kuumbwa kwake.
Mwanzo wa dhambi ulitoka katika mwanamke,
na kwa sababu yake sisi sote tunakufa.
Yoshua bin Sira 25:24