Wauguzi wapatiwa mafunzo ya kuhudumia watoto njiti, Kwimba

Wauguzi wapatiwa mafunzo ya kuhudumia watoto njiti, Kwimba

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
726
Reaction score
953
Wahudumu wa afya wanaotarajia kutoa huduma kwenye jengo jipya la Watoto njiti lililopo Hospitali ya Wilaya ya Kwimba wamepewa mafunzo maalum ya namna bora ya kutumia vifaa vya kisasa na kuwahudumia Watoto njiti ili kuwasaidia Watoto hao na Mama zao kupata huduma bora.

Akiongea na @AyoTV_ Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga Hospitali ya Taifa Muhimbili na Daktari Bingwa Mbobezi wa Watoto Wachanga Dkt. Martha Mkony ambaye ni Mkufunzi wa mafunzo hayo amesema “Mafunzo haya ya Mama na Mtoto yamekuja wakati sahihi kwa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba ambako ipo katika hatua ya kufungua jengo maalum la kuhudumia Watoto wachanga, imejumuisha watoa huduma Hospitali ya Wilaya ya Kwimba na watoa huduma za afya kwenye vituo vya afya vyenye Wagonjwa wengi Wilaya ya Kwimba na Misungwi”

“Watafundishwa kwa nadharia na elimu ya vitendo ili kujifunza njia madhubuti kabla hajaenda kwa Wagonjwa aweze kutoa huduma nzuri, Doris Mollel Foundation wamegusa na wamegusa juhudi za Rais Samia kuhakikisha Watoto wanapata huduma za afya bora, wodi hii ni ya kwanza nchini ambayo imekidhi vigezo vya WHO”

Kwa upande wake Elizabeth Honela amnaye ni Mfanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba na mmoja wa wanaopatiwa mafunzo hayo amesema “Tupo kwenye mafunzo ya utoaji huduma kwa Watoto njiti kipi kipya ni zero separation kati ya Mama na Mtoto tunaamini baada ya mafunzo tutakuwa vizuri kwenye kuhudumia Watoto, tumepokea jengo la Doris Mollel Foundation (@dorismollelfoundation) kwa jengo lile muhimu lenye vifaa vyote tofauti na hapo awali hakutokuwa na haja ya kuwapa Wagonjwa rufaa”

Mafunzo hayo yametolewa kwa usimamizi wa DMF chini ya uwezeshwaji wa WHO ambapo Wauguzi hao wametolewa na Serikali ya Tanzania.

Mafunzo hayo yametolewa kwa usimamizi wa DMF(@dorismollel) chini ya uwezeshwaji wa WHO na Wauguzi hao wametolewa na Serikali.
 
Back
Top Bottom