Wauawa wakipokea misaada ya Ramadhan

Wauawa wakipokea misaada ya Ramadhan

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
260
Takriban watu 78 wameuawa katika mkanyagano katika shule moja katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa wakati wa ugawaji wa misaada kwa ajili ya Ramadhani, maafisa wanasema.

Kanda za video kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha matukio ya fujo baada ya tukio hilo katika eneo la Bab-al-Yemen mjini humo. Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba mamia ya watu walimiminika katika shule hiyo kupokea michango ambayo ilikuwa takriban $9 (£7) kwa kila mtu.

Waasi wa Houthi wameendesha mji huo tangu walipoiondoa serikali mwaka wa 2015. Wale waliohusika na usambazaji huo wamezuiliwa na uchunguzi unaendelea, wizara ya mambo ya ndani ilisema.

Msemaji wa wizara hiyo alilaumu mkanyagano huo "usiokuwa na mpangilio" wa kutoa fedha bila kuwa na utaratibu na viongozi wa eneo hilo.

Watu wengi pia walijeruhiwa huku 13 wakiwa katika hali mbaya, afisa wa afya mjini Sanaa alisema

Shirika la habari la Associated Press linawanukuu watu wawili walioshuhudia ambao walisema wapiganaji wa Houthi walifyatua risasi hewani katika kujaribu kudhibiti umati wa watu, wakionekana kugonga waya wa umeme ambao ulisababisha mlipuko.

Hii ilisababisha hofu iliyosababisha kukanyagana, waliongeza.

Tukio hilo lilitokea wakati wa siku za mwisho za mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhani, ambao huadhimishwa na kipindi cha mfungo.

Yemen imeathirika na mzozo ulioongezeka tangu mwaka wa 2015, wakati Wahouthi walipochukua udhibiti wa maeneo makubwa ya magharibi mwa nchi hiyo.
 
Ala kafurahi,wajiandae kwa bikra 70
Huna akili ,kuleta udini katika vifo vya mamia ya watu kosa waliokufa ni watu wa dini nyingine ?

Nyinyi ndio wale wale hata Uturuki ilipopata tetemeko mkaanza kashafa za kidini ,usiombe itokee katika familia yako halafu mtu aje kukufanyia kebehi ,kuna wakati ufike ujiheshimu.

Watu wahuni wakatili walikosa huruma wameua raia wenzao watoto na wanawake tena katika mwezi wa Ramadhan bila hatua yeyote halafu wewe unaleta udini wako upo sawa kichwani ?
 
muwe mnawakosoa hao masheikh wapunguze kuropoka mwishowe ndo mtu akikosoa mnasema mdini kumbe mwenzio hayupo huko
 
Back
Top Bottom