Habari wanabodi,
Naunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha si tu kuwa wanarudisha heshima ya elimu ambayo kwa kipindi kirefu ilikuwa imepotea, bali pia wanarejesha ubora wa huduma zitolewazo kwa wananchi na wafanyakazi kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote wamepitia mafunzo husika ktk kutoa huduma waifanyayo.
Zoezi la uhakiki wa vyeti ambalo limeshapita lilihusisha na kubaini watumishi wenye vyeti vya kughushi na vyeti kutumika zaidi ya mara moja miongoni mwa watumishi wa umma. Naihakikishia serikali kuwa inawezekana ikawa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana ktk kuwabaini watumishi wenye vyeti vya fake (Havipo ktk database ya NECTA) na ndo maana hata orodha yao ilikuwa ni kubwa sana. Lakini ukija upande wa watumishi wanaotumia vyeti ambavyo sio vyao, hakika serikali haijaweza kufanikiwa hata kwa asilimia 40. Hii ni kwa sababu kuna kundi kubwa la watumishi wa serikali ambao wanatumia vyeti vya watu ambao si watumishi wa serikali (Wafanyabiashara au watumishi ktk sekta binafsi).
Wito:
Naomba nitoe wito kwa mawaziri wanaohusika, kama nia yao ni hiyo niliyoitaja hapo juu, basi wakae na waangalie ni namna gani wanaweza kuwabaini watumishi wa umma ambao wanatumia vyeti vya watu wengine ambao si watumishi wa umma. Namna ambayo inaweza kuwa na ufanisi wa hali ya juu ktk kulifanikisha hili, ni kuharakisha zoezi la utoaji wa vitambulisho vya utaifa, na miongoni mwa taarifa zitakazojazwa basi ziwe ni taarifa za elimu za sekondari zikiambatana na kujaza index number ya form four/six.