Watumishi wa ofisi za serikali mjiheshimu

Password

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
777
1,082
Habari wana JF.

Juzi nilienda pale ofisi za kwenye ofisi za DAWATI LA JINSIA NA WATOTO pale Karibu na kituo cha polisi iringa Karibu na soko kuu.basi baada ya kufika pale tukaingia ndani ila hatukukuta mfanyakazi tukaa kidogo kusubiri ndipo mmoja akatokea na kutuaita akasema "nyie ingieni" tukaingia.

Kufika ndani tukakuta watu watatu wote wanawake mmoja alikuwa katulia wawili walikuwa wanahangaika na simu, sisi tukawasalimia wote, huyo mmoja ambaye ndio alikuwa wa kulishughulikia tatizo letu ni anakera kuliko maelezo kwanza baada ya kumsalimia alijibu huku anachati kwenye simu, baada ya kujibu alikaa kama nusu dakika ndo anauliza Shida yetu ni Nini.

Hapo napo anauliza huku anachati tulivyoanza kujieleza tatizo lililotupeleka pale basi anasikiliza tena anaokota simu anachati alafu anaweka chini Dah mpaka hapo nikawa nimedic kinoma ila hakuna namna maana Huyo ndo mhudumu mwenyewe.

Basi baada ya kumweleza akanza kujibu hapo ameweka simu chini akaotota rula zile za Revlon,anajibu huku anachezea rula Mara aipeleke kichwani, Mara anaisogeza mdomoni Mara anaanza kusogeza stepler iliyokuwa pale mezani kwa kutumia rula aliyoishika muda wote huo anafanya yote hayo akiwa anaongea na sisi yaani ndo anatujibu hapo hajamaliza kuongea tena kaokota simu kachati kaneno tena karudi kwetu hapo sasa akaanza kuingizia na story zingine anasimulia huku kawageukia wenzake wanacheka kale kakicheko pendwa ka kinadada.

Yaani Dah kama tusingekuwa wawili pale nisingeelewa kabisa kwa maana nilisha poteza uelewa tangu Mara ya kwanza kabisa ambapo alijibu salamu huku anachati, nilikuwa namwangalia tu nikimshangaa.

Basi baada ya hapo ikaonekana ishu yetu itabidi twende ustawi wa jamii basi tukatoka pale tukaanza kwenda kwenye ofisi za ustawi wa jamii duhh yaani huku sasa ndo baba lao kwanza kwakuwa sisi tulikuwa wageni pale ikatubidi kuulizia ofisi zilipo hapa kila mtumishi tuliyemuuliza alikuja na jibu lake yeye kila mmoja alieleza anakokujua yeye watu tukabaki njia panda mwingine alitueleza nje kabisa akitutaka tuvuke barabara yaani kama sio mtumishi mmoja hivi sijui ingekuwaje huyo ndio akatuambia "ni jengo lile pale"(huku akionyesha kwa kidole) niliwashangaa sana walioeleza sehemu tofauti akati jengo lenyewe lilikuwa mbele yetu kabisa na wao ni watumishi wa muda mrefu na bado najiuliza sijui ni makusudi au.

Basi sasa baada ya kufika kwenye hizo ofisi tukakuta foleni ya kufa mtu nasi tukaunga apo baada ya muda foleni ikapungua kabisa na hadi nikabaki mimi na mwenzangu wawili tu huku tukijua kwamba kuna mtu aliyetutangulia akitoka tutaingia.

Kweli yule mtu alitoka ila tulipotaka kuingia tukaambiwa tusubiri hapo tulisubiri tena kama dakika arobaini na tano huku tukisikia vicheko tu,hapo mpaka tunakuja kuingia foleni huku nje ilikuwa imejaa kama tulivyo ikuta na zaidi baada ya kuingia huko ndani kumbe muda wote tunasubiri pale kwenye foleni wao walikuwa wanakula ofisi ina vyombo vichafu vingine ni uji halafu chumba kidogo kina meza tatu hata sehemu ya kupishana hakuna, sasa hawa nao ukimfuta mtu mmoja akuhudumie ukimuuliza swali anajibu yeyote yule wengine utani mwingi hadi wanasahau mada hii ilikuwa ni mida ya saa tano na nusu ahhhh nilichoka yaani dahhh,hivi kwenye ofisi za serikali kuna muda maalumu wa kula au ni muda wowote tu sio siri hii siku iliniudhi

Hapa lengo langu ni kwamba watumishi wa umma wajirekebishe.
 
pole sn.

una kipaji kikubwa cha kuhadithia... umetisha

kwani ulikuwa na tatizo gani?
Mkuu tatizo langu ni kwamba mzazi hataki kulipa ada na hko ustawi wa jamii wananiambia serikali inamtambua mtt mwenye umri chini ya miaka 18 zaidi ya hapo anauwezo wa kujihudumia...sasa cjawaelewa maana kawaida kwa nchi hii mtt anaanza darasa la kwanza na miaka 7 mpaka kumaliza kidato cha nne anakuwa na miaka 18 je kuanzia kidato cha tano mtt ajisomeshe au vipi
 
Mkuu tatizo langu ni kwamba mzazi hataki kulipa ada na hko ustawi wa jamii wananiambia serikali inamtambua mtt mwenye umri chini ya miaka 18 zaidi ya hapo anauwezo wa kujihudumia...sasa cjawaelewa maana kawaida kwa nchi hii mtt anaanza darasa la kwanza na miaka 7 mpaka kumaliza kidato cha nne anakuwa na miaka 18 je kuanzia kidato cha tano mtt ajisomeshe au vipi


ndio maana walikupotezea.

sheria inatambua mtoto ni chini ya miaka 18 kiumri...
 
pole aisee. ujinga huu upo sana ofisi za serekali kwasababu watu wanapewa kazi kwa kujuana tu huyo dada hayuko professional coz hana wasiwasi ya kupoteza kazi. ujinga huu huwezi kukuta kwenye ofisi za mashirika private coz ukileta uzembe watu wataomba kuonana na boss wako. inasikitisha hasa ukianglia watumishi wa serekali mishaara yao tunailipa sisi wenyewe
 
Back
Top Bottom