Watuhumiwa wa Ugaidi wagoma kufika Mahakamani wakilalamikia upelelezi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF

Watuhumiwa 52 kati ya 61 wanaokabiliwa na kesi 15 tofauti za ugaidi wamegoma kufika Mahakamani Arusha, wadai upelelezi unatumia muda sana. Hakimu aahirisha kesi hadi April 25, 2017.

freds.png


sxsx.png

SABABU ZA KUGOMA

Watuhumiwa hao walipofika mahakamani tarehe 28Machi 2017 walisema kuwa ndiyo itakuwa mwisho wao kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa Jamhuri utakapo kamilisha upelelezi wao.

Katika malalamiko yao walisema kuwa wamekuwa wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya kusingiziwa.

Aidha walisema wamekuwa wakipewa ahadi hewa na mkuu wa upelelezi kuwa angeshughulikia shauri hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba linaleta ukakasi kwa wananchi.

Hakimu Mfawidhi Nestory Baro wa mahakama hiyo aliwataka watuhumiwa kuwa na subira wakati wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na aliwataka kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifanya utaratibu wa kumtafuta mkuu wa upelelezi na kuzungumza naye.
 
Ila kweli jamani miaka minne upelelezi haujakamilika duh hatari
Sasa Sijui alionana nae mkuu wa upelelezi akaongea nae'!,
 
Back
Top Bottom