Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 522
- 2,940
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru *Ndugu Jerry Cornel Muro,* Amesema watu wote watakaotuhumiwa ama kujihusisha na vitendo vya ubakaji na kuwapachika mimba watoto wilayani humo watakiona cha mtema kuni kuwa hawatapata *dhamana pindi wakikamatwa na kufikishwa polisi* *Dc Muro* Ametoa kauli hiyo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha katika *maadhimisho ya miaka 20 Ya shirika la kimataifa la Compasion International* la kuhudumia watoto waishia katika mazingira magumu.
Kwanza tunafarijika kuona namna unavyopambana kutokomeza ubakaji na mimba kwa Dada zetu ,hakuna mtu anaye mtetea mbakaji ,ila lazima tujue una pambana vita kwa njia inayokeuka sheria na taratibu za nchi yetu.
Unaposema mtuhumiwa wa ubakaji au mtia mimba hatopata dhamana unatumia kifungu gani cha sheria ?
Maana tuna sheria zinazotuongoza nchini kwetu ,na tunajua unazijua.
Dhana ya kutokuwa na hatia (Presumption of innocence) ,ibara ya 13 (6) (b) ya 1977 ,sura No.2 kama ilivyofwa marejeo 2002 inasema " Ni marufuku kwa mtu yeyote aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo,mpaka hatakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo " sasa wewe unanyima mtu dhamana ikiwa ni mtuhumiwa tuu ,Kama amesingiziwa ? ,Kwanini usiache Mahakama ndio iamue Kama kuna sababu za kutoa au kuzuia dhamana kutokana na grounds mezani?
Alafu lazima tujue huku ni kuingilia muhimili wa Mahakama Mh.Muro, ukisoma ibara ya 107 (A) (1) ya katiba yetu 1977 inasema "mamlaka ndio yenye kauli ya mwisho ya utoaji wa haki katika jamhuri ya Tanzania"
Sasa Mh.Muro ,unazuia dhamana kwa sheria ipi ? ,Wewe ndio chombo cha mwisho ?
Kama wahanga wanapewa vitisho , mtuhumiwa akipewa dhamana ,bado vyombo vya sheria vipo mawakili wa waserikali(state attorneys) kwa ushahidi waombe Mahakama kuzuia dhamana kwa kusikia na upande wa utetezi juu ya vitisho kwa wahanga kutoka kwa mtuhumiwa,mbona taratibu zipo wazi .
Sasa Mh.Muro wewe unazuia dhamana kwa sheria zipi au kwa by-laws za ofisi ya DC wa arumeru [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Tuheshimu sheria,pia hongera kwa kuwa na nia ya kupambana dhidi ya mimba na ubakaji.
Abdul Nondo .