Watu wawili wajeruhiwa kwa mapanga Kasulu kutokana na mgogoro wa shamba

Ava Sancez

Member
Jan 27, 2017
33
50
vlcsnap-2017-03-22-12h08m18s099.png


Familia kumi zimekimbia nyumba zao katika kijiji cha Muganza wilayani Kasulu mkoani Kigoma baada ya baadhi ya wakazi wa kijiji hicho kujeruhi watu wawili kwa mapanaga na kufyeka zaidi ya ekari tano za mazao mbalimbali kutokana na mgogoro wa ardhi.

vlcsnap-2017-03-22-12h03m26s304.png


Vurugu katika kijiji hicho zimezimwa na Jeshi la polisi nakuwakamata watu watano ambapo waathirika wa tukio hilo wamesema chanzo ni mgogoro wa shamba linalomilikiwa na Adolph Mfumya,ambapo wavamizi pamoja na kujeruhi wakazi wa kijiji hicho wamefyeka ekari tano za mazao .

Kaimu mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Marco Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe amesema serikali itachukua hatua kwa wote waliohusika na uhalifu ambapo amewataka wananchi wa kijiji hicho kutoendeleza mgogoro huo.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom