Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Watu wawili wamefariki dunia akiwemo mwanamke mmoja mjamzito baada ya kuzama katika mto Lihanje wakati wakivuka mto huo kwa kutumia mtumbwi kwenye kijiji cha Nambendo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya Songea ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo Bw. Pololeti Kamando Mgema akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ametembelea eneo yalikotokea maafa hayo na kuwataja waliofariki dunia kuwa ni mama mjamzito Wande Shimbi ambaye mwili wake umeshapatikana Muhando Muhando ambaye mwili wake bado haujapatikana.
Jitihada za kuutafuta mwili mwingine bado zinaendelea huku vifaa vya kutafutia vikiwa kikwazo huku mkuu wa wilaya Bw. Pololeti Kamando Mgema akiwataka wananchi kuendeleza jitihada za kuutafuta mwili wa Muhando Muhando.
Chanzo: ITV