Shehe nielewe vizuri.Una elimu gani wewe? Okay hao wanaomaliza form six wamefundishwa na watu gani? Unavyougua unaenda hospitali au unatumia miti shamba? Barabara unazopita zimejengwa na akina nani?
Vizuri mkuu ila hao madokta, manesi wanaotibu watu huko wangetoka wapi kama wasingefika huko vyuo vikuu, Kuna professional mbalimbali bila vyuo vikuu watapatikana kweliShehe nielewe vizuri.
Nimeanza kwa kusema si kama napinga Elimu,La! Hasha.
Watu mnatakiwa muwe na maono.kesho yako haijengwi na wewe kwenda Chuo.
Au kwa kutokwenda University si mwisho wa maisha.
Mfano.
Aliye sababisha Hospitali ya KCMC iwepo,marehemu Mch.Stephano Mosha Elimu yake ilikuwa ni ya Form four tu.
Leo hii kuna mijitu ina ma Phd,blah blah,Je? Wamefanya kitu gani?
I Like you point.Nimekusoma mtoa mada lkn lazima baadhi ya watu waende vyuo vikuu otherwise System zitasimama
Bila chuo kikuu nani atatengeneza bia,saa,simu,Atm,Mpesa,Ndege,magari,madawa,usindikaji nani atabuni formula.Shule ni muhimu mno.Sema sio kila mtu ni wa kwenda chuo kikuu
Unaweza kusoma mpaka ukamaliza vyuo vyote ukarudi na kujifanya unabuni miradi,miradi yenyewe eti small scale agriculture.. Ha ha ha ha ha hii ndo bongo dsm
Hujanielewa!!!
Nimeanza kwa kuandika...''si kwamba napinga Elimu,La! hasha''....
Ulichoongea ni kweli kabisa.. Sema hapa tutapinga kutokana na madhara ya hiyo elimu tuliyopata.. Hasa wale ambao wamekalia madawati ya vyuo vikuu miaka 3/4 na hawajapata ajira..
Nina mdogo wangu,, kamaliza kidato cha sita mwaka 2014 akapata div3 ya point 11.. Hakupata Chuo kwa kozi aliyokua anataka (udaktari).. Nikamshauli aje jeshini then atasoma baadae.. Akapinga sasa hivi anaangaika mtaani wakati wale wenzake wapo TMA.. kiukweli haina haja ya kuunga Chuo direct wakati hakuna mustakabali mbeleni.. Sikwenda Chuo ila nimeajiriwa.. Plan.. Plan
bonge la ujumbe sema tu hujasomeka kwa watu wengi! ni vyema na haki mtu aka focus kwenye fun yake na sio kufuata mkumbo. kama unakwenda chuo kwa lengo la kuendeleza fun yako its okay lakini kama unakwenda chuo kwa fun isiyo yako umepotea kabisaaa... kwani utajutia mda na pesa ulizo poteza. "Do the right thing in the right place at the right time"