Watu wa zamani #14

kafumo

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
26
Reaction score
15
Hata katika mtu sio kila mahali pana hatari au unyeti ndio hivyo hivyo kwa kiumbe sayari dunia.

Kidole cha mkono kina kazi lakini kikikatwa na kutolewa mtu hawezi kupoteza uhai wake, hata katika sayari ya dunia kuna vitovu vingi vya nishati za kiroho lakini vinazidiana umuhimu katika kuwepo.

Kwa mtu kichwa ni kiungo muhimu sana kwenye uwepo wa uhai wa mtu na mwili wake, hata kwa sayari ya dunia kuna sehemu ya muhimu au takatifu zaidi kama ilivyo kichwa kwa mtu.

Pamoja ni ukweli kwamba haiwezekani kukuta pweza wamezaliana na wanaishi mazingira ya mlimani pasipo na maji.
Hata katika maji sio kila mazingira utampata pweza.
Basi kila eneo huwa na vitu vyake kutokana na jinsi na namna lilivyo kwa asili yake.
Pia ni suala gumu kukuta jicho kwenye mguu bali ni rahisi zaidi jicho kuwepo kichwani kwa kiumbe.

Unaweza kuona kichwani ni patakatifu pa namna gani na ikiwa pweza kiumbe wa baharini na ni ngumu kupatikana sehemu pa nchi kavu pasipo na bahari na hata baharini sehemu za namna flani ndio pweza wapo, basi sehemu patakatifu pa sayari kiumbe dunia pata kuwa na vitu vya namna gani.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…