Watu wa zamani #11

kafumo

Member
Joined
Aug 30, 2026
Posts
26
Reaction score
15
Kabla mtu yoyote haja anza kujadili habari ya uwepo wa dini ni muhimu atambue kuwa dini inaongelea mambo ya kiroho.

Kiroho ni mambo ya sirini, kulingana na habari za watu wa kale sirini ndio pakwanza kisha ndio bayana inafuata.

Kiroho ni habari ambayo ndio hiyo inahusisha nguvu za kiroho kwa maana ya nguvu zisizo onekana na macho ya nyama ambazo ni dhahiri zinatenda.

Kuachana na watu wa kale mambo ya nguvu za kiroho ni mambo ambayo yapo hata sasa, na ni baadhi ya watu ndio wanaelewa habari hii vizuri na ni baadhi ya watu wachache wasio elewa habari hii ya nguvu za kiroho.

Watu hawa baadhi wanao elewa habari ya nguvu za kiroho na utendaji wake wanafahamu habari ya matambiko, na wanaelewa kuwa sio kila mahali pana stahili kufanyia matambiko, pia wanaelewa kabisa matambiko hujibu kwa muda na wakati sahihi.

Lakini pia watu hawa baadhi wasio elewa habari ya nguvu za kiroho sio makosa yao na wengine ni makusudi kabisa maana wanatumia vitu wasivyo vielewa wanaishi maisha wasiyo yaelewa pia na hawataki kuelewa kama hawaelewi.

Wanafahamu kuwa simu za mkononi na simu zingine hazifanyi kazi bila minara ya mawasiliano, lakini wengi wanaweza wasielewe kuwa sio kila mahari panafaa kuwekwa minara.

Watu wanao fahamu habari ya nguvu za kiroho wanaelewa kuwa sio kila mahali ni kitovu cha nguvu za kiroho sahihi kwa ajili ya matambiko na pia wanaelewa kuwa sio kila mahali panafaa kwa ajili ya minara ya mawasiliano.

Wakati huo huo hawa watu wasio elewa habari ya nguvu za kiroho wengi wao hawajui kuwa sio kila mahali pana stahili kuwekwa minara ya mawasiliano wao wapo wapo tu !.

Huu ndio utofauti wa jamii ya watu wanao elewa habari ya nguvu za kiroho, na wale wasio elewa habari ya nguvu za kiroho.
 
The age of reason, watu hawataki imani... sijui wa miaka ijayo itakuwaje!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…