General Galadudu
JF-Expert Member
- Nov 7, 2015
- 1,868
- 2,199
Leo nakuja tofauti kabisa na nilivozoeleka, naomba sana msaada wa ufafanuzi juu ya hii ndoto niliyoota leo na nimeamka bado imekisonga sana kichwa changu...... kwny uzao upande wa mama yangu walikuwa 6, wanaume wawili ambao ni wajomba zangu na wanawake wanne ambao ni mama zangu wakubwa kwa maana ya kwamba mama aliyenizaa ni wa mwisho kuzaliwa kwa hiyo wale wengine wote ni wakubwa kwake.
Wale wajomba zangu na mama zangu wakubwa wote wamefariki, na mama mzazi pia amefariki tarehe 30/08/2012......lakini sasa....... wa mwisho kufariki ni ma mkubwa ambae ni wa kwanza kuzaliwa, yeye alifariki tarehe 20/08/2013 hapo unaona kuna utofauti kdg tu wa mpishano kwny vifo vyao kati ya mama na ma mkubwa (na nilipopata mtoto wangu wa kwanza wa kike miaka mingi kidogo iliyopita nilimuita jina la huyo mama yangu mkubwa, wakati huo bado wote walikuwa hai) kwa sasa hivi sina mtu wa kumuoneshea kuwa yule ni mjomba wangu au yule ni mama yangu mkubwa/mdogo au mzazi, wote ardhi imemeza...... sasa ndoto iko namna hii.
Ucku wa kuamkia leo eti nimeota nipo mimi, mama na huyo ma mkubwa ambae ndo wa kwanza kuzaliwa kwao na amefariki wa mwisho, tumeenda kumsalimia dada yangu ambae ni mtoto wa huyo marehemu mama yangu mkubwa yeye ameolewa na diwani, tuliandaliwa chakula lakini kilichelewa kidogo kwa hiyo mama mkubwa akaanza kusinzia...... kwa kabila yetu, mtoto wako ukimpa jina la mzazi wako basi kwa yule mzazi inakuwa automatically kwamba yeye ni mwanao, kwa hyo nikamchukua mama mkubwa aliyekuwa anasinzia ambae ni mtoto wangu nikambeba miguuni, halafu mama ambae ni mdogo wa huyo eti akaanza kulia anasema kwamba na yeye nimbebe.......!!
Jamani hicho ndo kimenichanganya sana naomba kujua maana ya hii ndoto, maana tangu wafariki haipiti siku mbili au tatu naota mambo mbalimbali kuhusu mama mzazi, wakati mwingine naota tunaongea, tunataniana nk. sishangai sana..... maana mimi kiasili napenda sana mizaha, kwa hiyo haikuwa ajabu kukuta namtania mama kwa utani wa kawaida tu, lakini kwa ndoto hii ya leo imenichanganya kwa kweli.