beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Leo ni siku ya Kifua Kikuu Duniani inayoadhimishwa kila tarehe kama ya leo.
Huo ni ugonjwa uliopo katika sehemu nyingi nchini na mataifa mengi duniani na hasa masikini, hivyo ni vyema umma ukaufahamu kwa kina namna ulivyo na athari zake.
Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na aina mbalimbali za bakteria wadogo na kwa kawaida, kinaathiri mapafu na kina uwezo wa kuathiri sehemu nyingine za mwili.
Pia husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia hewa, wakati mgonjwa anapokohoa, kupiga chafya au mate yake yakiwa hewani. Ni maradhi yanayoua zadi ya asilimia 50 ya wagonjwa.
Dalili zake za kawaida ya kutambua maambukizi ni mgonjwa kuwa na kikohozi sugu, kukohoa damu, homa na joto kali kwa mgonjwa, huku akitokwa na jasho jingi usiku na kupungua uzito.
Namna ya kutambua maambukizi katika utatibibu kumna njia kadhaa. Mojawapo ni kwa kutumia mashine X ray kifuani kwa mgonjwa, pia matumzi ya darubini za maabara kuchunguza vimelea mwilini.
Ili kuzuia kifua kikuu maarufu kama TB, ni muhimu kwa mgonjwa kupimwa na ni lazima watu wapimwe ugonjwa na kufanyiwa chanjo.
Kifua kikuu kimegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kuna kifua Kikuu Kikali ambacho kimezoeleka kama TB na kifua Kikuu Tulivu.
TB hudhuru kwa bakteria kushambulia mwili na mfumo wa kinga unaposhindwa kuwazuia.
Watu wenye kifua kikuu kikali kwenye mapafu, wanaweza kumuambukiza bakteria mwingine aliye karibu anapokohoa, kupiga chafya au kutema mate, mtu aliye karibu anaweza kuwavuta bacteria hao.
TAKWIMU
Hadi mwaka jana nchini Tanzania wanakisiwa watu 120,000 kuwa wagonjwa wa kifua kikuu na taarifa ya Shirika la Msaada la Marekani (USAID), linasema kuwa mwaka 2007, vifo vilivyotokana na ugonjwa wa kifua kikuu kwav wastani wa klila mwala vilikuwa 32,000 nchini Tanzania.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 zilizoathiriwa sana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa takwimu za WHO, kwa dunia nzima mwaka 2012 watu milioni 8.6 waliambukizwa Kifua Kikuu na watu milioni 1.3 kati yao walifariki, wengi kutoka katika nchi zinazoendelea.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha mwaka jana, Tanzania ilikuwa nchi ya 15 kati ya 22 ambazo zimeathiriwa sana na ugonjwa huo. Mwaka 2012, watu milioni 8.6 waliambukizwa ma kati yao watu milioni 1.3 walifariki.
Katika ulingo wa Kimataifa, asilimia 98 ya waathirika wa Kifua Kikuu wanatoka katika nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzaniau.
TB NA UKIMWI
Pia kuna unaoonyesha kuwa, asilimia 30 ya vifo vya watu walioathirika na Ukimwi vinatokana na kifua kikuu.
Taarifa zinaonyesha kuwa kati ya asilimia tano na 10 za watu wenye virusi vya Ukimwi wanaugua TB. Pia, asilimia 40 wanaougua kifua kikuu wana virusi vya ukimwi.
Kwa mujibu wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donald Mmbando, hadi mwaka jana Tanzania ilikuwa nchi ya sita barani Afrika kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu.
Takwimu zinaonyesha hadi mwaka 2013, kulikuwapo zaidi ya wagonjwa 65,000 wa kifua kikuu na utafiti wa mwaka 2012 ulionyesha kuwa idadi kubwa ya watu wenye umri zaidi ya miaka 50, wapo hatarini kupata ugonjwa huo.
Takwimu za kimataifa zinaonyesha takribani watu milioni 1.5 duniani, wanafariki kwa ugonjwa kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo vinatokea nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Tanzania ambayo imo katika ukanda huo, inadhika nafasi ya 22 kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Kifua Kikuu duniani. Kundi la nchi hizo ndizo zinachangia asilimia 80 ya wagonjwa wa kifua kikuu duniani.
Nchini Tanzania kumekuwepo ongezeko la wagonjwa kutoka 11,000 mwaka 1980 hadi 63,892 mwaka 2012, huku utafiti ukianisha kwamba asilimia 30 ya vifo vya watu walioathirika na ukimwi vinatokana na TB.
Pia inaelezwa kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kuwa na wagonjwa wengi kwa takwimu za mwaka 2012 Dares Salaam (13,983), Mwanza (5,946) na Shinyanga (4,074).