Watu 20 wauawa hotelini Somalia

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Waziri wa usalama wa ndani nchini Somalia amesema watu 20 walifariki baada ya hoteli mbili maarufu za ufukweni kushambuliwa mjini Mogadishu.

Bw Abdirisak Omar Mohamed ameambia idhaa ya Kisomali ya BBC kwamba watu wengine 20 walijeruhiwa baada ya hoteli za Lido Sea Food na Beach View kushambuliwa Alhamisi jioni.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la al-Shabaab limedai kuhusika kwenye shambulio hilo.

Mabomu yaliyotegwa kwenye magari yalilipuka kabla ya wapiganaji kuingia hotelini na kuanza kufyatulia watu risasi.

Wapiganaji hao waliwashikilia mateka wageni na wafanyakazi wa hoteli kwa muda wa saa nane.

Maafisa wa serikali ya Somalia wamesema kwa sasa maafisa wa usalama wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa hoteli hizo na mhusika mkuu wa shambulio hilo amekamatwa.

Waziri mkuu wa Somalia, Omar Abdirashid Ali Sharmarke, ameshutumu mashambulio hayo na kuyataka kuwa ya “kikatili”.


Chanzo: BBC
 
Hayo niauaji ya Kipumbavu yasiyo na tija kwa mstakabali wa amani ya Kudumu nchini Somalia. Suala ni je hivi vikundi vyenye silaha nchini Somalia na kwinginepo wanaotumia mwavuli wa dini kuua watu vitaendelea kutenda hayo hadi link? Kwa faida ya nani? Na mwisho wa yote kitokee nini? Ni wakati mwafaka sasa dunia nzima kwa umoja wake kusimama na kulaani kwa nguvu moja mauaji ya aina hiyo , iwe Nageria , Libya , Misri , Syria, Kuwait, Iraq , Pakistan nk nk. Hakuna sababu yoyote iwayo ile itakayo halalisha mauji
 
Back
Top Bottom