Watu 120,000 huongezeka Dar kila mwaka

Watu 120,000 huongezeka Dar kila mwaka

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,056
Reaction score
1,086
JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa miji mikubwa nchini inayoathiriwa na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Ili kukabiliana na tatizo hilo Tanzania inahitaji dola za Marekani milioni 500 kila mwaka kwa ajili ya kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri miji mikubwa likiwamo jiji la Dar es salaam.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaojadili kuhusu makazi, uharibifu wa mazingira pamoja na mabadiliko ya tabianchi ulioandaliwa na Chama cha Wataalamu na Wadau wa Mazingira Duniani (IAPS) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Ardhi, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alisema katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya, ipo haja ya wataalamu wakatafuta suluhu ya matatizo hayo.

“Kwa sasa Jiji la Dar es Salaam linakabiliwa na changamoto ya ongezeko la watu 120,000 kila mwaka, tatizo ambalo linakwenda sambamba na tatizo la makazi, maji safi na salama, usafi wa mazingira na tatizo la ajira,” alieleza Samia.

Katika Mkutano huo wa kwanza kufanyika nchini na unahudhuriwa na nchi wanachama 16 kutoka mabara manne Makamu wa Rais aliwataka Chuo Kikuu Ardhi kwa kushirikiana na wataalamu wengine kwenye mkutano huo, kuja na maazimio na mapendekezo yatakayoisaidia nchi kutatua tatizo la mipango miji, makazi holela, miundombinu, utawala na usimamizi wa mazingira ili kufikia ajenda ya ukuaji miji ya mwaka 2030.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa alisema uharibifu wa mazingira kwa Jiji la Dar es Salaam ni mkubwa kutokana na ujenzi holela, uchimbaji wa mchanga, kuziba mifereji ya maji na uharibifu wa kingo za bahari.

Profesa Liwa alisema wajibu wa kwanza wa kutunza miji na mazingira ni wa jamii yenyewe na serikali kupitia Sera ya Mipango Miji ihakikishe wananchi wanajenga kwenye maeneo yaliyopangwa na kuboresha maeneo ambayo yamejengwa kiholela.

Kwa upande wake, Dk Nathalie Jean-Baptiste kutoka IAPS ambao ni waandaaji wa mkutano huo, alieleza kuwa chama hicho kina jumla ya wanachama 400 duniani kote.

Alisema wajumbe katika mkutano huo watajadili mifano hai kutoka baadhi ya miji kama Dar es Salaam na Mwanza ambayo pia imeathirika kutokana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, lakini pia mapendekezo yatakayotolewa kwenye mkutano huo yatasaidia kupambana na matatizo ya mafuriko, makazi holela na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi mijini.

Habari Leo
 
Waje tu ila waishi kwa akili, wasilete tu zile ratiba za bush huko asubuhi chai viazi, mchana ugali nyama,jioni wali marage.

Dar mahesabu aisee, mpaka usiku utapata supu ya kongoro, ngozi au bichwa la ngombe kwa jero na maandazi, mihogo inakaangwa jioni unashushia juisi ya 200 siku imeisha.
 
Vijana wa mikoani wanakuja mjini sasa sijui nani atalima?
 
Huwa najiuliza yaani idadi ya watu waliopo dar na kila mtu daily ana fanya excreesion..hizo disposal sijui zinakuwaje?
 
Watarudi wenyewe kijijini ,,,,kwa hali hii ya kifedha only few will make it
 
Kwa taarifa tu life ya dar ni nafuu in terms of chakula na utafutaji pesa za kujikimu via biashara ndogondogo za uchuuzi but ni magumu sana kwenye ishu ya malazi,mkoani hakuna pesa na vitu ikiwemo msosi ni bei ghali mfano dar kipande cha tikiti au ndizi moja mbivu unapata kwa sh.mia mkoani hakuna kitu kama hiyo
 
Inawezekana kweli au kuna mtu anaweza amini maafisa wa mipango miji wasijue concept ya urbanization na potential cities Tanzania zenye pull factor.

Vitu vingine uitaji taasisi ya kimataifa kukwambia miji yenyewe inatakiwa kuwa na mipango yake ya muda mrefu kukabiliana na changamoto za urbanization, they are just a bunch of lazy ppl that's all there is to it sio kwamba eti hawajui.
 
Mkuu hapana hivi ushafika Mbeya ukajionea Debe la viazi mviringo linauzwa kiasi gani? Nenda Tukuyu angalia ndizi, maparachichi, mahindi, kabichi ni bei gani? Shuka Kyela angalia Mchele ama nenda Ubaruku
 
naamini wanaokuja tanzania ni wengi sana kuliko hiyo idadi na wanao ondoka ni wengi sana maaana
 
Waje tu ila waishi kwa akili, wasilete tu zile ratiba za bush huko asubuhi chai viazi, mchana ugali nyama,jioni wali marage.

Dar mahesabu aisee, mpaka usiku utapata supu ya kongoro, ngozi au bichwa la ngombe kwa jero na maandazi, mihogo inakaangwa jioni unashushia juisi ya 200 siku imeisha.
Kwa hali iyo msiwalaumu "wanaume wa dar"
 
Wangapi wanaondoka kila siku? Kwa jinsi Dar inavyopigwa madongo nilitegemea wanaoingia wawe 0 wanaotoka 120,000
 
Mkuu hapana hivi ushafika Mbeya ukajionea Debe la viazi mviringo linauzwa kiasi gani? Nenda Tukuyu angalia ndizi, maparachichi, mahindi, kabichi ni bei gani? Shuka Kyela angalia Mchele ama nenda Ubaruku
But hoja yangu inajikita kwenye centres za mikoa,huko countryside ni dhahiri bei zitakuwa ni simple sana
 
Inawezekana kweli au kuna mtu anaweza amini maafisa wa mipango miji wasijue concept ya urbanization na potential cities Tanzania zenye pull factor.

Vitu vingine uitaji taasisi ya kimataifa kukwambia miji yenyewe inatakiwa kuwa na mipango yake ya muda mrefu kukabiliana na changamoto za urbanization, they are just a bunch of lazy ppl that's all there is to it sio kwamba eti hawajui.
Inawezekana kabisa mipango ipo ila utekelezaji wake unahitaji fedha.
 
Back
Top Bottom