Watu 12 wauwawa katika shambulio la kwanza la 'IS' nchini Iran

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
ISIS.jpg

Mashambulio mawili ya kujitoa mhanga katika Bunge la Iran na kwenye eneo la kaburi la kiongozi wa kidini Ayatollah Khomeini kwenye mji mkuu wa Iran, Tehran, yamesababisha vifo vya watu 12 na wengine wengi kujeruhiwa.

Mashambulio hayo katika jumba la Bunge, kwa sasa inaonekana imemalizika, baada ya masaa kadhaa ya kuzingirwa, huku milio ya risasi ikisikika.

Mlipuaji mmoja wa kujitoa kufa aliyekuwa amevalia vilipuzi, alijilipua katika eneo hilo la kumbukumbu na kaburi la Khomeini.

Maafisa wa usalama wa Iran wamefaulu kuzima shambulio hilo.

Mashambulio hayo yalifanyika vipi?

Watu waliokuwa wamejihami na bunduki aina ya AK, waliingia ndani ya majengo ya Bunge, Jumatano asubuhi.

Picha kutoka mahala pa tukio zilionyesha operesheni kali ya walinda usalama, huku wanajeshi wakizingira bunge.

Milio mikali ya risasi zilisikika.

Kundi la Islamic State (IS), limekiri kutekeleza mashambulio hayo, ambayo ni ya kwanza kutokea nchini Iran.

IS imeweka picha mtandaoni, inayodai kuwa ni ndani ya majengo ya Bunge.

Duru zinasema kwamba washambuliaji hao wenye silaha waliingia Bungeni kupitia lango la raia, wakivalia kama wanawake.

Runinga ya taifa ya Iran baadaye iliripoti kuwa, washambuliaji wanne walioingia ndani ya majengo ya Bunge, wameuwawa na walinda usalama.

Mamlaka kuu nchini Iran inapinga dhana kuwa, kunao watu waliozuiliwa matenga ndani ya majengo hayo ya Bunge.

Shirika la habari la Iran IRIB lilimnukuu mbunge mmoja akisema kuwa kulikuwa na washambualiaji kadha ndani ya majengo ya bunge waliokuwa wamejihami na bunduki aina ya AK-47.

Shirika hilo la habari lilisema kuwa walinzi wawili walijeruhiwa.

Ripoti zinasema kuwa ufyatuaji risasi katika kaburi la Ayatollah Khomeini ulifanyika wakati mmoja.

Chanzo:BBC swahili
 
Sunni wameshambulia shia, haina neno! Chakushangaza ni ndani ya ramadan
 
Sunni wameshambulia shia, haina neno! Chakushangaza ni ndani ya ramadan
Inashangaza sana kwa kweli! Mauwaji mengi ya magaidi hufanywa ndani ya Mwezi Mtukufu. Unahitajika utafiti kujua ni kwanini; labda ni kipindi cha makafara? Au labda kutokana na swaumu wanakuwa "wamezama" sana kutetea wanachokiamini? Ila Iran naye amesapoti sana hivi vikundi vya kishenzi asidhani wengine hawawezi ku-revenge kwa mtindo ule ule. Labda atajifunza kitu.
 
Back
Top Bottom