Watoto wawili lakini sina hamu na ndoa, namtoroka

MTWA

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
1,166
168
Huyu mtu wangu tuna miaka 8 naye watoto wawili, nimesafiri miaka 4 na kurudi mara 2 home japo mawasiliano yalikuwa daily tuwe waaminifu, ila baada tu ya kurudi nimekuta mabadiliko kibao:

1. Nikipofika tu nilimpa zawadi ya simu mpya, ikasumbua na kuombwa nimsaidie, ghafla nikafika katika msg video ya ngono imetumwa na kijana wa mlango wapili wa mahali tulipanga zamani. Yeye kajibu unanitamanisha. kumuuliza mkali na kumwambia ukweli na maana, akashusha pressure kaugua.

2. Hii iliniuma: Kila siku amechoka, anaumwa, kitandani hayupo na jikoni hayupo, ila kuchat, so busy,ikipigwa simu na mdogowe nikapewa nami nisalimu mtoto akanisimamia kuchukua simu haraka nikasema nione nini! Kumbe wanachat mambo yote ya mchana na usiku na mwalimu mwenzie na mwingine ambaye pia alimwomba wafanye mapenzi weekend moja, naye hakukemea zaidi ya kuuliza muda kumuuliza yaleyale.

3. Huyu mwingine ni rafikiye mwalimu pia ambaye ni mwanasoka mwenzangu. ila pia anasimuliwa mambo ya home yeye mimi nitajua baadaye. Wife akisafiri jamaa anapokewa na kugawiwa zawadi kwanza ni mtu anapewa upendaye zote za home kwangu ila juzi nakuta msg ya wife "poa my" jamaa"okay luv u, ufute sms usijisahau" nikamkanya, akawa mkali nikamwambia sasa nimechoka akashusha pressure tena kuamka taarifa kwa jamaa ni mengi sana sasa sitaki kusema naye hivi sasa yupo harusini jamaa kampeleka na gari mi nipo safari.

Sasa natafuta hela siku ikifika labda nimwache nisijemuua kwa pressure, ili nilee watoto kwa remote na yeye akiwa hai, kwasababu yake sina hamu tena na ndoa na mambo yake ila najiuliza nina gubu au yeye ananikosea kweli.
 
Chukua hatua mapema, hakuna mapenzi wala uaminifu tena hapo. Hamaaa
hatua za mapema ni zipi,.maana mwanzo ndo nilijarib kumkumbusha, ila matokeo ni ukali na ukimwelekeza naye ana shida hiyo.hofu atarudia mengine aje kushusha pressure moja kwa moja
 
Mnatukatisha tamaa ya kuoa.........!!
ucjali fundisho
ukimpenda usikubali kuwa nao mbali wayasingizia oooh wanaume nyinyi.... kumbe wao ndo hawana subira
wepesi sana kudanganyika hawa
 
Wanaume ndio maaan tunawahi kufa ila nimegundua sehemu kubwa tunajitakia wenyewe kuwahi kufa.

Mtu unaina ujinga wake kila siku na una ushahidi wa kutosha sio mwaminifu bado unambembeleza kila siku?

Achana nae mapema, utatunza watoto, mpe uhuru wa kuishi peke yake at.ombeke huko kwa uhuru maana ndio shida yake. Usijali cha kushusha presha wala kupandisha, kama angejua hayo asikuchepuka.

Uumize kichwa kutafta pesa bado nyumbani kuna kunguru anakuumiza na wewe unambembeleza kwa nini usife mapema.

Achana nae kabisa.
 
Huyu mtu wangu tuna miaka 8 naye watoto wawili, nimesafiri miaka 4na kurudi mara 2home japo mawasiliano yalikuwa daily tuwe waaminifu. ila,.baasa tu ya kurudi nimekuta mabadiliko kibao:
1.nikipofika tu nilimpa zawadi ya sim mpya, ikasumbua na kuombwa nimsaidie, ghafla nikafika katika msg video ya ngono imetumwa na kijana wa mlango wapili wa mahali tulipanga zamani. yeye kajibu unanitamanisha. kumuuliza mkali na kmwambia ukweli na maana, akashusha pressure kaugua.
2. hii iliniuma: kila siku amechoka, anaumwa, kitandani hayupo na jikoni hayupo. ila kuchat, so busy. ikipigwa simu na mdogowe nikapewa nami nisalim mtoto akanisimamia kuchukua simu haraka. nikasema nione nini! kumbe wanachat mambo yoote ya mchana na usiku na mwal mwenziye na mwingine ambaye pia alimwomba kumt.mba.. weekend moja. naye hakukemea zaid ya kuuliza muda
kumuuliza yaleayale.
3. huyu mwingine ni rafikiye mwl pia ambaye ni mwanasoka mwenzangu. ila pia anasimuliwa mambo ya home yeye mimi nitajua baadaye. wife akisafiri jamaa anapokewa na kugawiwa zawadi kwanza. ni.mtu anapewa updaye zote za home kwangu. ila juzi nakuta msg ya wife "poa my"
jamaa"okay luv u, ufute sms usijisahau"
nikamkanya, akawa mkali. nikamwambia sasa nimechoka. akashusha pressure tena. kuamka taarifa kwa jamaa. ni mengi sana sasa sitaki kusema naye hivi sasa yupo harusini jamaa kampeleka na gari mi nipo safari. sasa natafuta hela siku ikifika labda nimwache nisije muua kwa pressure. ili nilee watoto kwa remote na ye akiwa hai. kwa sababu yake sina hamu tena na ndoa na mambo yake.
ila najiuliza nina gubu au yeye ananikosea kweli!
samahani msg ndefu mno!
duh, kimeo changu kina afadhali aisee!
 
kumbe, mara zingine kushea ili kujua matatizo yetu hayazidi wengine. ukikaa nayo utafreeze bure
matatizo yako yanaweza kuwa madogo kuliko ya jirani yako unayefikiri anafiuraha! kusanya ushahidi wa kutosha unapomuonya ukiwa wazi kwa mtazamo wako wa kugawana mbao kama hana mpango wa kubadirika tabia.
 
Huyo mdada kaona presha ndio fimbo wala hafai binafsi namchukia mtu awe mpenzi au mume kabisa kutoa siri za ndani na kuzipeleka nje maana hapo ni kuchoreka grade one huyo ita wazazi wake wamchukue wenyewe usije mpeleka wewe akajipandishia presha .... Pole
 
ucjali fundisho
ukimpenda usikubali kuwa nao mbali wayasingizia oooh wanaume nyinyi.... kumbe wao ndo hawana subira
wepesi sana kudanganyika hawa
Usigeneralise .... Afu umenikumbusha mbali na hiyo ID yako ....
 
Ashajua udhaifu wako ndiyo maana anakuendesha hivyo... Kampumzishe kwanza, hakuna cha matumizi wala salaam, alafu hao wanaomuona mzuri wakati yupo kwako wamuhudumie huko huko alipo... Uone kama ajashika adabu...
 
kumbe ukishusha presha unasamehewa eeeh!
siyo mimi mshusha pressure ni yeye ukimpa ukweli na implication zake. sasa kama nitaendelea ivo na yeye hajui kama ni kosa, si nimwua. nimeamua kumwacha ila nafikiri kuwa kama mimi hili siyo gubu nimwache kwa amani.
 
Ashajua udhaifu wako ndiyo maana anakuendesha hivyo... Kampumzishe kwanza, hakuna cha matumizi wala salaam, alafu hao wanaomuona mzuri wakati yupo kwako wamuhudumie huko huko alipo... Uone kama ajashika adabu...
kwani unatujua nini, nikihisi kama hayo. sababu yeye anaona kama mimi poa sana. anyway sipo ivo, ila napanga kutomsgushia pressure kimoja. watoto watanililia bure
 
Back
Top Bottom