Wakiwafanza watoto
Washindwalo kutambua, kwa uzoba kuwajaa,
Kila wakiwachezea, wao huwa ndio juha,
Vijembe wakivitia, wakawa wanaotaniwa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Uongo waliojaa, huwa wanatambuliwa,
Kweli wakiikataa, nguo zao hujivua,
Uchi tuakjionea, hadharani walokuwa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Kiinimacho watia, huku wanajichubua,
Lengo wakikusudia, hawana la kufanikiwa,
Husuda waliojaa, chuku inawakamia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Gizani waliokaa, nuru inawakimbia,
Maluni kawaingia, sawa wanajionea,
Hadi wakakosa haya, utupu kujitambia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Yao yazidi chukiwa, na kisasi kuwekewa,
Mwanzo kidogo vikawa, vikizidi vikajaa,
Mafuriko yaingia, na wao hawajajua,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Gharika inawajia,wao ujuzi watia,
Na mbwembwe kujifanyia, wajao jiondokea,
Lao la kuandikiwa, kwa viumbe kuhadaa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Laana waichagua, nyumbani kwenda kukaa,
Na nuksi kuivaa, njiani wakatembea,
Siku inapowadia, wote tutashuhudia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Maskini wasojua, wajifanya wanajua,
Njia walio0potea, upofu waukataa,
Viziwi wasiosikia, wajifanya wasikia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Ububu waukataa, ovyo wajipayukia,
Hata siri kuzitoa, kaumu wakazijua,
Hawana la kuambiwa, laana waliolaaniwa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Hauwezi kuzuia, hicho walichoandikiwa,
Hadi neno kutimia, mengi tutayasikia,
Msikae kushangaa, kuvuna ni kujiandaa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Washindwalo kutambua, kwa uzoba kuwajaa,
Kila wakiwachezea, wao huwa ndio juha,
Vijembe wakivitia, wakawa wanaotaniwa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Uongo waliojaa, huwa wanatambuliwa,
Kweli wakiikataa, nguo zao hujivua,
Uchi tuakjionea, hadharani walokuwa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Kiinimacho watia, huku wanajichubua,
Lengo wakikusudia, hawana la kufanikiwa,
Husuda waliojaa, chuku inawakamia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Gizani waliokaa, nuru inawakimbia,
Maluni kawaingia, sawa wanajionea,
Hadi wakakosa haya, utupu kujitambia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Yao yazidi chukiwa, na kisasi kuwekewa,
Mwanzo kidogo vikawa, vikizidi vikajaa,
Mafuriko yaingia, na wao hawajajua,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Gharika inawajia,wao ujuzi watia,
Na mbwembwe kujifanyia, wajao jiondokea,
Lao la kuandikiwa, kwa viumbe kuhadaa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Laana waichagua, nyumbani kwenda kukaa,
Na nuksi kuivaa, njiani wakatembea,
Siku inapowadia, wote tutashuhudia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Maskini wasojua, wajifanya wanajua,
Njia walio0potea, upofu waukataa,
Viziwi wasiosikia, wajifanya wasikia,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Ububu waukataa, ovyo wajipayukia,
Hata siri kuzitoa, kaumu wakazijua,
Hawana la kuambiwa, laana waliolaaniwa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!
Hauwezi kuzuia, hicho walichoandikiwa,
Hadi neno kutimia, mengi tutayasikia,
Msikae kushangaa, kuvuna ni kujiandaa,
Wakiwafanza watoto, wao huwa taahira!