Watoto wa kike vyuo vikuu jichungeni

musomatarime

New Member
May 14, 2016
2
0
NUKUU “...Tanzania inayo dhamira ya dhati ya kuhakikisha kuwa inaendeleza kuhimiza suala la usawa wa kijinsia na kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake katika nchi yetu. Kamwe hatutarudi nyuma katika suala hili. Niko tayari kushirikiana na viongozi wa nchi zingine katika kufanikisha utekelezaji wa dhamira hii katika mataifa yote barani Afrika”. (Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marangu, Kilimanjaro 05 Machi, 2012).

jitihada za kufikia usawa wa kijinsia na kuwapatia uwezo wanawake kupitia programu mbalimbali za maendeleo zimeendelea kuimarika. Hii inatokana na Serikali kutambua kuwa usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ni masuala muhimu kufikia maendeleo. Maeneo ambayo yamezingatia usawa wa kijinsia ni pamoja na nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali, mfano, uwakilishi wa wanawake katika Bunge, halmashauri za Wilaya na taasisi mbalimbali za Serikali. Aidha, udahili wa wanafunzi katika shule za msingi, sekondari na vyuo umezingatia usawa wa kijinsia. Pamoja na mafanikio hayo, bado zipo changamoto ambazo zinakwamisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia. Mpaka sasa bado zipo mila, desturi na imani potofu ambazo zinaendelea kuathiri haki ya wanawake katika masuala ya kutoa maamuzi na kushika nafasi mbalimbali za uongozi. Aidha, suala la mimba na ndoa za utotoni zinachangia katika kudhoofisha maendeleo ya elimu ya wanawake

kuna baadi ya wanaume ambao hawajali jitihada hizi .tunaomba taasisi zinazohusika na masuala ya elimu a juu kuliangalia hili hasa pale wanaume wanaosoma chuoni kwa daraja la la juu la elimu wanavyowarubuni watoto wadogo wanaosoma vyuoni shahada za chini.

Mfano kwenye chuo kimojawapo ambacho nitakitaja baadae wapo wanaume wanawarubuni watoto mfano ni Dakari mmoja ambae yeye anawarubuni watoto kuwa aawapa kazi nzuri wanapomaliza na pia atawaoa na akishampata anampeleka nyumba ya kulala wageni .

Kinachosikitisha ni kuwa huyo daktari ni muathirika anawasambazia wanachuo ukimwi.

Daktari huyo anatembea na vipimo vya kupimia ukimwi akishamfikisha binti ndani anampima kwanza kama ana maambukizi ya ukimwi kabla ya kumuingilia kinyume na maumbile .

Mchezo huo amekuwa akiufanya kwa watoto kadhaa kadhaa wa kike na kuwatelekeza kila wanapohoji au kukataa mchezo huo mchafu ambapo kitendo hicho kimekuwa kinawaumiza kisaikologia .
 
Back
Top Bottom