Watendaji halmashauri fanikisheni mradi wa PS3 mjikomboe kiutendaji

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
HALMASHAURI 97 za mikoa 13 ya Tanzania Bara, zimechaguliwa kutekeleza Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Miradi hiyo imeshazinduliwa katika mikoa 10 na halmashauri 20 katika mikoa hiyo kati ya halmashauri hizo 97.

Halmashauri zote zitakazofaidika na mradi huo, zimeshapatiwa mafunzo na nyingine sita zitapata mafunzo wiki hii juu ya namna ya kutekeleza mradi huo. Mradi huu wa PS3 unalenga kuboresha mifumo ya utendaji kazi kwa ufanisi kwa halmashauri husika na kuondoa matatizo yanayokabili halmashauri hizo.

Vigezo mbalimbali vilitumika katika kupata mikoa na halmashuri hizo zitakazonufaika na mradi huo. Ingawa Tanzania ina mikoa mingi, ni mikoa 13 tu ndiyo itakayofaidika na mradi huo na hiyo ni bahati kubwa kwa mikoa hiyo. Kimsingi, mradi huo ni miongoni mwa miradi bora iliyowahi kutekelezwa nchini kupitia shirika hilo la Marekani la USAID.

Mikoa ambayo imebahatika kuingia katika mradi huo unaotekelezwa na Taasisi ya Abt Associates Inc ikiwa na washirika kutoka ndani na nje ya Tanzania ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa na Shinyanga.

Kutekelezwa kwa mradi huo katika mikoa hiyo, naweza kufananisha na mtoto wa masikini ambaye amepata ufadhili wa kupatiwa elimu bure. Hivyo, kinachotakiwa ni jitihada tu za kijana huyo na utayari wake wa kusoma kwa bidii ili ajikwamue katika ujinga na umasikini na pia jamii yote inayomzunguka, itakuwa imefaidika na kusoma kwake.

Mikoa inayotekeleza mradi huu ni vyema sasa ijiweke katika kundi la mtoto wa masikini, aliyepata msaada wa kusomeshwa kwa ajili ya kujikwamua. Halmashauri mbili kutoka kila mkoa, ndizo zilizoanza kutekeleza mradi huo.

Sifa moja kubwa ya kuwa wa kwanza ili kuingia katika mradi huo ni mahitaji ya mradi huo kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo. Ni lazima kusimamia utawala bora na kushirikisha wananchi katika miradi hiyo.

Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ngazi za serikali za mitaa, kutawezesha rasilimali kutumika kwa uwazi na pia kutawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kupanga, kufuatilia na kutoa matokeo katika kila sekta.

Endapo kama mradi huo utakuwa umetekelezwa ipasavyo katika maeneo husika, basi itakuwa ni suluhisho kwa wale waliokuwa wakipata hati chafu. Mradi utaimarisha mifumo, hasa ya rasilimali watu, kwa kuongeza mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi.

Mradi utatoa mafunzo juu ya usimamizi wa rasilimali fedha kwa kuongeza pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.

Aidha halmashauri zitakazotekeleza mradi huo, zitafaidika na uimarishaji wa mifumo ya mawasiliano, kwa kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini na matumizi ya takwimu kwa wadau. Utafiti tendaji ni moja ya nyenzo muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia.

Tafiti hizo zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa. Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini. Hivyo wito wangu kwa watendaji wa halmashauri na mikoa ni kujitoa vilivyo kutekeleza mradi huo ili uwe chachu ya maendeleo na kutoka kule ambako miaka nenda rudi halmashauri husika zilikuwapo. Kila mmoja awajibike ipasavyo kuhakikisha mradi huo unafanikiwa. Halmashauri zilizoanza kutekeleza mradi huo, ziwe walimu kwa halmashauri nyingine.
 
umeeleza juu juu sana hasa kwenye point ya faida za huo mradi kwa halmashauri zilizo teuli, binafsi mbali na kutoelewa faida za mradi huo lakini bado hujaniambia ni kiasi gani kitatolewa kwa kila halmashauri, faida zake na kwa nn mikoa hiyo na halmashauri hizo pekee ndizo zilizo chaguliwa!!/
 
Back
Top Bottom