WATANZANIA WAZALENDO
Kwa wale Watanzania wasiotanguliza itikadi za vyama vyao, imani za dini zao. Watanzani wanaoweka mbele maslahi mapana ya taifa letu la TANZANIA tukutane hapa tujadili mustakabali wa taifa letu bila kufungwa na imani au itikadi zetu.
Taifa letu linakabiliwa na viongozi wasiojua vipaumbele na maono yetu.Hawajui Tanzania inahitaji nini na tutapataje tunachokihitaji. Ikiwa hatujui tunachohitaji si rahisi kukitafuta,kwa kuwa hatutakuwa na mikakati wala mipango .Matokeo yake nchi imekuwa inaendeshwa ndivyo sivyo. Mathalan tumejiwekea sera ya kuifanya nchi yetu iwe ya uchumi wa viwanda .
Lakini kila kukicha tunafanya mambo ya kukinzana na azma yetu.
Kabla ya hili tulikuwa na “kilimo kwanza” hivi leo hatujui tumefanikiwa kiasi gani, tumekutana na changamoto zipi tumeweza au tumeshindwa kuzishughulikia vipi changamoto hizo.
TUFANYE NINI KUBADILIKA?
Tuanze hapa kujadiliana
"Kwa Maslahi ya Taifa".