Ukwelimtupu
Member
- Nov 21, 2011
- 36
- 13
Nimekuwa nikiumiza kichwa mara nyingi pale ninapotembelea makampuni mbalimbali haswa makampuni ya kigeni ambayo yanafanya shughuli zake hapa nchini. Viongozi wa juu wa makampuni haya wengi ni wageni (expatriates) na Watanzania waliowengi wanashikilia vinafasi vya chini chini tu. Mara nyingi makampuni haya yamekuwa yakitoa sababu kwamba Watanzania hawana ujuzi na uwezo wa kutekeleza majukumu ya kazi za juu kwenye makamupuni haya. Sababu hii ina ukweli flani mathalani kwenye makampuni yanayojihusisha na uchimbaji madini, utafiti na uchimbaji wa gesi asilia na sekta ya nishati. Ila inakuwaje kazi zote hadi uhasibu, uajiri na utawala Watanzania wasiweze?
Serikali ya Tanzania kupitia taasisi zake; Wizara ya Kazi na Ajira, Idara ya Uhamiaji, TIC (Tanzaia Investment Centre) na Ofisi ya Waziri Mkuu, wameruhusu uingizwaji wa wageni kwenye kazi ambazo Watanzania wana ujuzi na uwezo mkubwa wa kuzifanya. Kwa mfano kuna umuhimu gani wa kumleta mfanyakazi wa kigeni awe Mhasibu? Salesman? Dereva? Ofisa Utawala?
Mara nyingi tabia hizi za kuingiza wageni nchini na kuwapa kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya imejikita sana kwenye makampuni ya watu wa jamii ya Kiasia kama vile wahindi.
Jambo wasilolijua viongozi hawa wa serikalini ni kwamba endapo Watanzania watapata fursa za kushikilia nafasi za juu kwenye makampuni yanayofanya biashara hapa nchini uchumi wa Tanzania utakuwa zaidi kwa sababu kipato wanachokipata Watanzania hawa watawekeza nchini. Mara nyingi wageni hawa hawana hulka ya kuwekeza nchini na matumizi yao hujikitakwenye chakula tu. Pia Watanzania wengi wanofanya kazi huwa na tegemezi wasiopungua wanne. Sasa jiulize endapo Watanzania kama watano watapata nafasi za juu za uhasibu ambazo zinawalipa wastani wa TZS 5,000,000 kwa mwezi ni familia ngapi zitakombolewa kutoka kwenye umaskini wa njaa? umaskini wa afya? umaskini wa kutopata elimu bora? nk. Inamaanisha kwamba familia tano zitakuwa zimepata maisha bora kutokana na watu watano tu walio na kazi nzuri ambazo wamezipata kutokana na usimamizi mzuri wa sera ya ajira.