Nihzrath
Member
- Jan 15, 2013
- 51
- 116
Huu ni mwaka wa uchaguzi, mamilioni ya watanzania watapaswa kumchagua kiongozi wao kwa muhula wa 5, kwa mihula mingi sasa watanzania hawajapata kiongozi mwenye weredi na uchungu wa maliasili za watanzania na mwenye upendo , mzalendo, kwao. Hivyo ifikie hatua inatosha watanzania wanahitaji kiongozi mwenye sifa hizi:
1.Kwanza lazima awe kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza, awe mchukia rushwa na mpinga ufisadi.
2.Ni lazima tuangalie historia yake uko nyuma, akiwa kiongozi sehemu yoyote ile, nini amewafanyia watanzania kuwaletea maendeleo, hapa aangliwe kwa utendaji wake wa nyuma.
3.Ni yule ambaye anapenda haki na mkweli,....tuachane na viongozi wenye kuongea sana bila vitendo.
4.Ni yule ambaye atakuwa na uchungu wa fedha za walipa kodi na hataweza kusafiri safiri kila mara nje ya nchi.
5.Ni yule ambaye atavirejesha viwanja vya michezo mikononi mwa umma, maana ni viwanja vyao lakini wamenyanganywa.
6.Ni yule aliye tayari kuwafungulia mashtaka, na kuwafilisi mafisadi wakiongozwa na mzee wa vijisenti.
7.Ni yule ambaye atalifanya jeshi la police kuwa mali ya umma na si mali ya chama tawala.
8.Ni yule ambaye ataruhusu mchakato wa katiba mpya, na kuruhusu maoni ya wananchi kuzingatiwa kwa maana ndio yenye tija kwa watanzania na kuitupilia mbali rasimu ya kifisadi iliyotungwa na fisadi.
9.Ni yule atakayekuwa na maamuzi magumu na yenye tija kwa watanzania, na si chama,
10.Msomi na mwadilifu, na mwenye uzalendo kwa taifa.
11. Ni yule atakayetoa amri kwa viongozi wote kutibiwa nchini, kwa kuboresha na kupunguza gharama za huduma za jamii.
13. Ni yule atakayefanya Mahakama kuwa chombo huru na chenye mamlaka kamili, na nguvu bila kujali cheo cha mtu.
14.Mcha mungu, na mwenye hofu ya mungu.
15.Ni yule atakayeruhusu vyombo vya habari kuwa uhuru tofauti ilivyo sasa.
16.Mwenye kujali maslahi ya nchi kuliko chama.
17.Hasiye mfanyabiashara, na mwenye kumiliki mali zisizo na shaka.
18.Mwenye kutimiza ahadi, mwenye kulinda haki na utu wa mtanzania,.
19, Ni yule ambaye ataruhusu mikataba yote muhimu kuwa wazi, ili watanzania wafahamu kufaidika kwao na wawekezaji.
20.Smart kichwani, smart kiutendaji, smart mavazi, smart moyoni.
Hakika huyu ndie tumtakaye......