Watanzania wahamasishwa kuwekeza kwenye teknolojia kwa kununua hisa za Vodacom.

Sudysoko

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
449
180
Habari zenu wanajamvi!?

Wakati tukiingia katika karne ya 22 inayohusisha maendeleo ya sayansi na Teknolojia watanzania wamehamasishwa kuwekeza katika sekta ya sayansi na Teknolojia kwani ndipo malengo ya Dunia yalipo.

Kuanzishwa kwa huduma za Simu 4G na 3G katika mitandao ya mawasiliano kumechangia kukuza matumizi ya Intaneti ambayo kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa ikwamisha kwa kiwango cha chini maendeleo ya mtandao nchini.

Ukitazama kwa sekta ya kimawasiliano nchini Tanzania imechangia asilimia 2.1 ya pato la Taifa kwa mwaka 2015 ambayo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 1 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 ukilinganisha na mwaka 2009.

Mitandao imekuwa ikikua kwa kasi kwa mtandao wa Vodacom wenye wateja zaidi ya milioni 12 umechangia kwakiasi kikubwa utoaji wa huduma zenye ubora ikufuatiwa na kampuni nyingine za Simu.

Kwa njia pekee ya Tanzania sasa ni kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano hasa kampuni za simu katika kununua hisa ili kuweza kukuza kiwango cha ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchi tayari kampuni ya Vodacom imeweka hisa zake sokoni kwa wateja wake kuweza kujipatia nafasi ya umiliki na kuchangia kukuza sekta ya mawasiliano nchini.

Soko la Data limekadiriwa kuwa na thamani ya takribani dola 966 milioni kwa mwaka 2016 -2017 na ukuaji wake ni takribani asilimia 6. Hii inachangia zaidi na ongezeko la wateja wa Intaneti

Watanzania mnatakiwa kujitokeza mstari wa mbele katika kuwekeza katika soko la hisa ndani ya kampuni ya Vodacom kwani kutaongeza upanuzi wa vipato vya kilasiku, pamoja na pato la Taifa katika ulipaji kodi ukiwekeza ndani ya Kampuni ya Vodacom katika kununua hisa kutaongeza nafasi ya kutanua zaidi soko la Ajira na kuifanya tanzania kuwa na tofuti ndogo kwa waliokosa ajira nchini.

[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG]
[HASHTAG]#KaziNiKwako[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Mtanzania[/HASHTAG]
9ad46bc260c035503c5f4110007001ac.jpg
 
Back
Top Bottom