watanzania tuwe wazalendo

watanzania tuwe wazalendo

chawade

Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
21
Reaction score
3
CHAMA CHA WANANCHI NA DEMOKRASIA
CHAWADE
Phone: +255 789113534, +255 715 039991
Mw/Chai – Matombo na Gombero (house No 28)
chamachawade@yahoo.com


TUSIDANGANYIKE!!!

Ndugu wananchi, leo napenda kujadili angalau kwa ufupi juu ya viongozi wetu wa vyama vya upinzani kama wana utofauti wowote na viongozi wa chama tawala (CCM).

Kabla hatujaendelea sana, kwanza tujikumbushe majukumu na malengo ya kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi, mfumo ambao Tanzania ulianza mwaka 1992 na hivyo kutoa nafasi ya kuanzishwa vyama vya siasa vikiwemo CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF, NLD, DP na vingine vingi na hadi sasa vimefika idadi sawa na wachezaji wa timu mbili za mpira wawapo uwanjani kwa maana nyingine 24.

Lengo na madhumuni ya mfumo huu au vyama vya upinzani ni kuleta fikra mpya, fikra tofauti, mtazamo tofauti na namna ya uendeshaji wa dola kama nchi kuleta mawazo na dhamira kinzani na ile ya chama tawala, sasa tujiulize swali dogo tu, je utofauti huo upo?

Tuangalie suala la demokrasia ndani ya vyama hivi. Vyama vya upinzani kama dira ya kuonyesha utofauti inabidi viwe ni vya mfano wa kuigwa. Suala la kubadirisha uongozi kadri ya katiba zao limekuwa ni changamoto kubwa, tumeshuhudia kiongozi mmoja anateuwa mwenyekiti kwa miaka nenda rudi, ina maana hakuna wanachama wengine wenye uwezo wa kuongoza. Sitaweza kuvitaja vyama hivyo, lakini ndugu wananchi kwa macho yenu mmekuwa mkiona na mtaendelea kuona. Chama tawala kimekuwa na mfumo na uchaguzi wa ndani ya chama kila baada ya miaka mitano na tumekuwa tukiona sura mpya zikichaguliwa.

Sasa kama vya upinzani ambavyo vinapewa kuonyesha njia vinakuwa vya kwanza katika kuiminya demokrasia, tuangalie matumizi ya fedha, vyama vyenye wabunge hupata ruzuku toka Serikalini. Tujiulize, je tangu vyama vya upinzani vianze kupata ruzuku toka Serikalini kuna siku tumesikia kikinunua na kupeleka hata msaada wa dawa hata kwenye zahanati moja? Je wamewahi kuchimba hata kisima cha maji hata kimoja tu cha mfano? Majibu mnayo wenyewe. Pamoja na misaada toka nje ya nchi lakini pamoja na misaada hiyo mambo ni yale yale na pengine mabaya zaidi: wanajilipa fedha lukuki pamoja na kununua magari ya kifahari ya chama sasa kuna mtindo wa kununua ndiege-chopa wengine wamenunua hadi choa tatu –zote hizo za nini na wananchi wanafaidikaje na chopa hizo? Haitoshi tu kusema hatuoni utofauti wao kabisa zaidi ya kutuhadaa.

Kuna mambo mengi sana tukiamua kuyachanguza tutaona ukweli kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawana utofauti wowote na wale wa chama tawala. Mambo wanayoyapigia kelele, wao ndio wa kwanza kutoyatekekeleza, kinacho fanyika ni sawa na kiini macho tu.
Tukiangalia pia uteuzi wa wabunge wa kuteuliwa ndani ya vyama vya upinzaji yaani ni majonzi tu. Tumeona dada, shangazi, binamu, baba mkwe, shemeji, mdogo mtu wakichanguliwa na kuingia bungeni kama wabunge wa kuteuliwa. Demokrasia ipo wapi hapo? Au demokrasia kwa chama tawala tu?

Tulisikia kelele nyingi sana Escrow! Escrow! Escrow kila kona na wengine wanapiga kelele ni kutoka vyama vya upinzani, lakini uchunguzi unaonyesha hadi viongozi wa vyama vya upinzani walipata mgawo huo sas hapo utofauti uko wapi? Mambo ni yale yale ambayo wananchi hatuyataki ndio nao wanayafanya.

Kwa mazingira haya ambayo tunayaona ndugu wananchi tuwe makini sana maana bila kuwa makini tutaendelea kudanganywa. Ni vizuri sasa tufumbue macho, tuwamulike ili wabadirike na kama hawata badirika na kuendeleza mambo yale yale na muda mwingine kuwafukuza ndani ya vyama wale ambao wanataka wanayo hubiri jukwaani yatendeke kadri wanavyohubiri basi tuamuwe moja nalo ni HERI YA SHETANI AKUJUAYE KULIKO YA SHETANI ASIYEKUJUA. Na ndipo tuseme TUSIDANGANYIKE.

Kwa hiyo sasa, ndugu wananchi napenda kuwajulisha kuwa mkombozi wa wananchi amekuja kutatua yale ambayo wengine wameshindwa na kuishia kuwa sehemu ya yala yanayofanywa na chama tawala. Chama kipya tumaini kwa wantanzania ni CHAMA CHA WANANCHI – CHAWADE.

Chama ambacho kinaamini katika misingi ya utawala bora, na utawala bora unauona ndani ya chama na ndipo tunakuwa na nguvu ya kusema kinachofanywa na wengine ni uvunjaji wa misingi ya demokrasia na utawala bora. Tunaamini katika nguvu ya wananchi wa kawaida, wakulima na wafanyakazi katika kuleta maendeleo na hivyo kuwpa nafasi ya kushiriki katika kuweka dola yenye kujali maslahi yao. Karibuni CHAWADE.


CHAWADE – KWA PAMOJA TUTASHINDA.


Shabiri Mpaka
Mwenyekiti Chawade.
 
Back
Top Bottom