Watanzania tuvumilie maumivu, neema inakuja! Ni Mapito kweli?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Bila shaka wakuu kila moja kwa hali ya maisha ilivyo hivi sasa sio swali la kujiuliza, sio kwa mfanyakazi, sio kwa mfanyabiasha, sio kwa mwanafunzi, mtota wala mkubwa,na hata watumishi wa Mungu! Kila moja amekata tamaa. Kiukweli kuna hali ngumu sana ya kimaisha mtaani na hakuna mwenyewe jibu la moja Kwa moja ni lini hali itatengamaa.Watumishi wa Mungu wanadai sadaka zimepungua makanisani na misikitini, wananchi wanadai hali ni ngumu hivyo kwao sadaka siku hizi ni kama mzigo.


Tuliambiwa sasa wale walioishi kama malaika wanatakiwa waishi kama shetani, sikujua ni kundi gani lilikua linazungumzwa hapa maana hata aliyeishi kama shetani zamani sidhani Kama kweli naye anaishi Kama malaika kwa sasa! Binafsi bado naona ni kama bado hakuna madiliko maisha ndio yanazidi kua magumu zaidi.


Wananchi wa maisha ya chini ndio hali inzidi kua ngumu zaidi, waliambiwa watapata unafuu wa maisha awamu ya tano lakini ndio kwanza maisha yanapamda mara dufu, ni zaidi ya miezi sita hivi sasa utawala wa awamu ya tano uko madarakani hakuna dalili yeyote ya unafuu wa maisha, walioishi kama sheitwan zamani kwa sasa wanakula walichohifadhi kibindoni na wengine wamekwishabadili mbinu za maisha.


Waalimu, Madaktari,wauguzi na wataalamu wengine wanaambiwa wasubiri zao zimesitishwa kwa muda kwanza kwa sababu ya matatizo ya watumishi hewa. Mimi sijui ukijumlisha idadi ya wakuu wa wilya na mikoa pamoja na idadi ya makatibu tawala na wakurugenzi nchi nzima utapata kiasi gani? Kwani si ndio watumishi wenyewe hao? Kwani nao si wanajaza mikataba ya ajira? tena wengine wanaajiriwa nafsi zaidi ya moja, kuajiriwa nafasi zaidi ya moja sio kutengeneza nafasi hewa ni nini? Nadhani hawa wakuu wa wilaya, makatibu tawala,wakuu wa mikoa na wakurugenzi ndio wanaoishi kama malaika.


Maumivivu ya kupanda kwa bei ya sukari, mafuta ya taa, ongezeko kubwa kwenye tozo za miamala ya huduma za fedha kwenye mitandao ya simu na mabenki! Mbaya zaidi mamlaka za serikali zinakinzana kwa kauli kuhusu gharama hizi, mwisho wa siku tutaambiwa kua tuishi hivyo hivyo kama tulivyozoea kama bwana moja alivyowahi kunena kwamba"hata kama wananchi watakula nyasi lakini ndege ya rais lazima itanunuliwa"


SWALI

Tuvumilie nini? Ni neema gani hiyo?
 
Back
Top Bottom