soweto85
JF-Expert Member
- Sep 6, 2016
- 301
- 247
Habari wanaJF,
Mimi binafsi nasikitishwa na kinachoendelea humu, hasa ikizingatiwa huu ni ulingo wa watu genius kwa asilimia kubwa. Malumbano haya hayatusaidii kitu zaidi ya kuwapa faida wanalolitakia taifa letu mabaya.
Tukumbuke rais ametoka kwenye uwaziri wa kawaida tu, Makonda alitoka kwenye Ukuu wa Wilaya, tena kwa muda mfupi sana. Sasa ukiangalia utendaji wa rais hutamuelewa isipokuwa urudi kihistoria kiutendaji kama Waziri wa Ujenzi. Msimamo wake hauna tofauti na sasa, kwani aliwawajibisha watu mpaka site huko huko, na kupachika hapo hapo mbadala wa aliyemtoa.
Kwa ufupi alipokua anaenda kutembelea mradi watu watu waliugua matumbo, na msimamo wake huo ulimfanya adumu kwenye Wizara ya Ujenzi kwa muda mrefu kuliko mawaziri wengine kwa sababu ni wizara ngumu. Na aliweza kudumu kwa sababu alikuwa na njia zake za kiutendaji.
Hawa aliowateua anaendelea nao kama hawatataka kumsoma staili yake ya uongozi, basi watatoka tu, wala mtu asijidanganye yeye ni mzizi kwenye chama. Tafuteni taarifa sehemu zote alizopitia kiutendaji mtafahamu staili yake ya kazi. Hata Makonda kwa tunavyomfahamu mh. ni kwamba nafikiri ni kwa sababu ya uthubutu wake kufuatilia matatizo ya watu mpaka uraiani, madawa, pamoja na matatizo mengine ambapo haijawahi kutokea hapo kabla. Ila staili zako usijeshangaa na wewe kutupwa nje.
Ni mchango wangu tu wa kifikra, masahihisho ruksa.
Wasalaam..!!