Kuna haja ya kupanua wigo wa uwajibikaji kwa makosa ya kazini ili kama taifa tupone.
Mkuu wa nchi anapomuamini mtu na kumteua alafu anaenda anaharibu hali ambayo inaitweza serikali, taifa, taasisi ya urais kama mamlaka ya uteuzi wake na pia zaidi rangi ya ngozi zetu.
Makosa ya mteule wa rais yanapothibitika kwa haki kuna haja ya kupanua wigo wa kuwajibisha wahusika ili waunganishwe pia wale waliomfanyia vetting na recommendations mtumishi (mtuhumiwa) kwa kumpelekea mteuzi wake jina la mtu ambaye kumbe hatoshi kwenye nafasi hiyo.
Wafuatao wametweza utumishi wa umma ambao mwajiri mkuu ni rais na hata kama wahusika waliteuliwa na taasisi za kimataifa (siyo rais) lakini bado taasisi hizo ziliomba vibali na recommendations kwa rais:-
1. Balozi Getrude Ibengwe Mongela, alihusika kwenye kashfa za ajira na zabuni akiwa Spika wa Bunge la Afrika.
2. Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu naye aliingia kwenye kashfa ya ujenzi wa nyumba ya ofisi na makazi ya Ubalozi wa JMT Italy. Prof. alifanikiwa ku-defend with cost Mahakamani (japo hakudai gharama) na hakurudishwa kwenye utumishi wa umma. Hadhi yake ya Ubalozi aliovuliwa alirejeshewa hatimaye baada ya Korti kutomkuta na hatia.
3. Balozi Dr. Asha Rose Migiro naye alipwaya katika nafasi ya kumsaidia Katibu Mkuu wa UN yeye Mhe. Migiro akiwa kama UN-DP-SG na M'kiti wa UN SDG.
4. Hivi sasa tena Balozi Hoyce Anderson Temu wa Geneva ameingia kwenye kashfa kubwa pia ambayo iko kwenye utaratibu wa kisheria ili haki itendeke. Soma kiambata.
Watz soka hatuwezi, riadha hatuwezi, ndondi tunapenya kwa bahati nasibu tu, mpira wa pete pia tunajitweza wenyewe.
Nafasi hizi za kimataifa huwa zina ushindani mkali sana ndani na nje ya nchi ya mhusika kwamba kuzipoteza kwa uzembe na tamaa kunahitaji hatua kali za kurejeshea wahusika sifa za utumishi wa umma.
Sina hakika kama Balozi Temu atathibitika kwa haki kuwa mhalifu mteuzi wake atamvua hadhi ya Balozi pia?
Sijajuwa Watz tunaweza kipi? Je, tutaweza lini kimataifa?
Michezo hatuwezi, siasa tunaboronga, uchumi shamba la bibi, ulozi tuko vizuri, kwenye kila kitu sisi ni Wasukuma tu. Baghosha!