Watanzania, Tuombe Risiti Tunaponunua bidhaa Tuongeze Makusanyo ya Kodi: Tujenge Taifa Letu

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,908
2,773
Ndugu zangu watanzania, Tanzania ni nchi yetu sote na maendeleo ya Tanzania ni maendeleo ya Kizazi chetu na vizazi vijavyo. Kodi ndio inaendesha shughuli za serikali na maendeleo ya kijamii na miundombinu mbalimbali kama ujenzi wa barabara, maji etc, inategemea uwezo wa serikali kutoa huduma hizo, tuwe wazalendo tudai risiti za ki electronic kila tunaponunua bidhaa.

Kwa njia hiyo tutaona kwa kiasi kikubwa tunapunguza utegemezi kutoka nje na shughuli za maendeleo tutafanya kwa pesa yetu ya ndani.

  • Mungu Ibariki Tanzania
 
Tangu mwaka huu uanze, hili ndo neno bora kabisa kuwahi kukutana nalo humu jf. Mtoa mada ni mzalendo wa kweli ambae ana uchungu na nchi yetu. Anaumia kuona maendeleo duni tuliyonayo. Moja ya sababu ni ukusanyaji kodi hafifu kutokana na uongozi mbovu wa awamu iliopita na pia sisi wananchi kutokuwa na utamaduni wa kudai risiti tunuapo bidhaa.

Maadam serikali ya awamu ya tano imeonyesha dhamira ya dhati kabisa katika ukusanyaji mapato na kuyatumia kuwaletea maendeleo watz , watz hatuna budi kuunga mkono serikali yetu kwa kudai risiti tununuapo bidhaa. Tukifanya hivi ndipo tunakuwa na uhalali wa kulalamika tuonapo maendeleo hayalingani na makusanyo.

Nami niongeze jambo moja. Wizara ya viwanda ianzishe kampeni maalum ya kuwahamasisha watz kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya serikali.

Lazima tutambue hatuwezi jivunia uhuru wetu ikiwa ni tegemezi.

Hapa hakuna ushabiki wa vyama vya kisiasa. Usipite bila ku- like post ya mtoa mada.

Mungu ibariki Tz.
 
Ngoja hili liwe moja ya maazimio yangu mwaka huu, KUDAI RISITI kwa ninunuacho na nichangiacho mchango wa pesa
 
Back
Top Bottom