Watanzania tujiandae 2020 sio mbali

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Kama tujuavyo Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya Kidemokrasia, na mwisho wa Uchaguzi Mkuu mmoja ni mwanzo wa maadalizi ya Uchaguzi Mkuu mwingine. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 yalibainisha kuwepo kwa mwitikio mdogo wa wapiga Kura katika baadhi ya maeneo, kama mnakumbuka mwaka 2015 kulikua na hamasa kubwa sana ya wananchi kuwa na shauku ya kuwapigia kura viongozi wanaowataka katika ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais.

Kati ya wapiga Kura 23,161,440 walioandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni wapiga Kura 15,596,110 ndio waliojitokeza kupiga Kura ikiwa ni sawa na asilimia 67.34. Wapiga Kura 7,565,330 sawa na asilimia 32.66 ya walioandikishwa hawakujitokeza kupiga Kura.

Hali hii imekuwa ikijitokeza katika chaguzi zilizopita tutazame mifano hapa

1. Mwaka 2000, waliojiandikisha ni 10,088,484 waliopiga Kura ni 8,517,998 (84.43%) na wasiopiga kura ni 1,570,886 (15.57%).

2. Mwaka 2005 waliojiandikisha ni 16,442,657 , waliopiga Kura ni 11,365,477(69.12%) Idadi ya wasiopiga Kura ni 5,077,180 (30.88%)

3. Mwaka 2010 waliojiandikisha ni 20,137.303 waliopiga Kura ni 8,626,303 (42.84%) na wasiopiga Kura ni 11,511,000 (57.16%).

4. Mwaka 2015 waliojiandikisha ni 23,161,440 waliopiga Kura ni 15,596,110 (67.34%) na wasiopiga Kura walikuwa 7,565,330 (32.66%)

MY TAKE: Kila Mtanzania anao wajibu wa kujitokeza kupiga Kura siku ya Uchaguzi, suala watu kuishia kujiandikisha tu na siku ya kupiga Kura hawajitokezi halikubaliki, wapo baadhi ya watu wanaamua kupuuzia au kuwakomoa wagombea kwa kutokwenda vituoni kupiga Kura, jambo hili sio tu linazuia mgombea asipate kura yako bali linasababisha watu wengine wakuchagulie kiongozi, Kura yako ni chanzo cha mabadiliko sote kwa pamoja tuliondoe kwa kuhakikisha kila aliyejiandikisha anapata fursa ya kupiga kura mwaka 2020.

KUPIGA KURA NI HAKI YAKO, MWAKA 2020 TUJITOKEZE KWA WINGI KUITUMIA VEMA HAKI HII.
 
Lakini ni kawaida Rais aliyepo madarakani amalize vipindi vyake vyote viwili, Unless otherwise proved with health problems si ndio jamani nadanganya jamani, msemakweli ni mpenzi wa mungu kabisa, so muache figisu zenu mapema
 
Yaaa atamaliza vipindi viwili kama atapata ridhaa ya watanzania
 
2015 kuna mambo kadhaa yalijitokeza ndio maana walijiandikisha wengi.

1. Ongezeko la watu hususan vijana wa 18+ hawa wengi waliozaliwa 90's
2. Umuhimu wa kadi ya mpiga kura ambayo inatumika kama ID, benki nk
3. Muamko wa wananchi pia kushiriki kwenye uchaguzi.

Sababu ya 2 inaelezea kwanini bado wengi hawakupiga kura
 
Mikutano ya kisiasa ifunguliwe....waache uoga... Vyama vitakufa...nchi yetu wote
 
Bora tuanze poll hapa hapa,inaeleweka kwa ccm Dk.Magu ndio atagombea 2020 kutokana na katiba yao,na pia kwa cdm Lowasa ndio anakubalika
 
Kama tujuavyo Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya Kidemokrasia, na mwisho wa Uchaguzi Mkuu mmoja ni mwanzo wa maadalizi ya Uchaguzi Mkuu mwingine. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 yalibainisha kuwepo kwa mwitikio mdogo wa wapiga Kura katika baadhi ya maeneo, kama mnakumbuka mwaka 2015 kulikua na hamasa kubwa sana ya wananchi kuwa na shauku ya kuwapigia kura viongozi wanaowataka katika ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais.

Kati ya wapiga Kura 23,161,440 walioandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni wapiga Kura 15,596,110 ndio waliojitokeza kupiga Kura ikiwa ni sawa na asilimia 67.34. Wapiga Kura 7,565,330 sawa na asilimia 32.66 ya walioandikishwa hawakujitokeza kupiga Kura.

Hali hii imekuwa ikijitokeza katika chaguzi zilizopita tutazame mifano hapa

1. Mwaka 2000, waliojiandikisha ni 10,088,484 waliopiga Kura ni 8,517,998 (84.43%) na wasiopiga kura ni 1,570,886 (15.57%).

2. Mwaka 2005 waliojiandikisha ni 16,442,657 , waliopiga Kura ni 11,365,477(69.12%) Idadi ya wasiopiga Kura ni 5,077,180 (30.88%)

3. Mwaka 2010 waliojiandikisha ni 20,137.303 waliopiga Kura ni 8,626,303 (42.84%) na wasiopiga Kura ni 11,511,000 (57.16%).

4. Mwaka 2015 waliojiandikisha ni 23,161,440 waliopiga Kura ni 15,596,110 (67.34%) na wasiopiga Kura walikuwa 7,565,330 (32.66%)

MY TAKE: Kila Mtanzania anao wajibu wa kujitokeza kupiga Kura siku ya Uchaguzi, suala watu kuishia kujiandikisha tu na siku ya kupiga Kura hawajitokezi halikubaliki, jambo hili sio zuri, tunatakiwa sote kwa pamoja tuliondoe kwa kuhakikisha kila aliyejiandikisha anapata fursa ya kupiga kura 2020 sio mbali.

KUPIGA KURA NI HAKI YAKO, MWAKA 2020 TUJITOKEZE KWA WINGI KUITUMIA VEMA HAKI HII.
2020 hakuna uchaguzi kutakuwa na tamasha tu la uchaguzi.Kwa mafuriko yale ya 2015,na mgombea wa mwendo kasi wa ukawa,kura hazikutosha,viroba marufuku Magufuli ataserereka tu juu ya ganda la ndizi hadi ikulu
 
Kama alichaguliwa maana yake ameshapata ridhaa ya watanzania si ndio jamani

Mi nachojua kila baada ya 5yrs tuna election! sasa kama Rais alieko madarakani atagombea tena haina shida si atapambana na wagombea wa vyama vingine na asiposhinda ndo basi tena.
 
2020 hakuna uchaguzi kutakuwa na tamasha tu la uchaguzi.Kwa mafuriko yale ya 2015,na mgombea wa mwendo kasi wa ukawa,kura hazikutosha,viroba marufuku Magufuli ataserereka tu juu ya ganda la ndizi hadi ikulu

Ha ha ha kabombe hii hataree Tamasha tena, tutakua na uchaguzi bana! watu tujipange tu uchaguzi utakua poa sana.
 
Kwa kwa tunavyokwenda mkuu,watu hajui cha kufanya,hakuna mawazo mbadala ibaki kula tu ruzuku hakuna anaewaza kujipanga
 
Back
Top Bottom