Watanzania Tuacheni Kushabikia misiba

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Hukuna kitu kinachoumiza kama kuondokewa na unaempenda au ambae ni tegemezi kwako.

Hivi sasa kumeibuka tabia ya kuanza kutafuta marehemu alichosema pindi akiwa hai na kukiweka mitandaoni.

Kumbuka unapoandika maneno mabaya kwa marehemu kumbuka wanandugu wanaowategemea na kuwapenda.

Kumbukeni swala la kifo ni siri ya mungu sio kwamba kumsema fulani ni mgonjwa ndio inapelekea kifo hapana.

Sisi watanzania tuna utani wa jadi kuanzia kwenye makabila, michezo na siasa kwa hiyo sioni ajabu mhaya kumtania msukuma, shabiki wa yanga kumtania shabiki wa simba na mfuasi wa chadema kumtania wa CCM.

Hebu tuwaachie marehemu wetu wapunzike.
 
Nashindwa kuku-categorize!!!!
Ni kweli umemaanisha "Hakuna kitu kinauma kama kuondokewa"???



Mwenyewe umejipiiiiiiiiiinda kuandika!!!!!
 
Sasa hivi tungekuwa na katiba nzuri kabisa bila ya kumwaga damu, sasa lile lizee likaichafua na kuichanachana katiba yetu, halafu wewe unataka tuliheshimu eti tu kwa sababu linaoza kaburini, acha hizo, sasa kuna hatari kubwa sana ya kumwaga damu ili kuipata katiba mpya na nzuri kama ile
 
Tunaweka tu kama kumbukumbu kwa vizazi vinavyokuja wajue tu marehemu aliwahi kusema ivi na ivi..
 
Mi siwaelewi wanaosema mwenzao atakufa mapema akati wao hawajui hatima yao.Mungu ndo apangaye kila kutu wanashindwa kukumbuka hilo
 
Siku zote malipo na hapa hapa duniani sasa muda wa malipo ndo huu muacheni mzee wa watu apumzike
 
Australia ukiwa na mbwa serikali inakulipa kiasi ili umtunze inavyotakiwa na siku mbwa huyo akifa basi familia huwa na majonzi na hupanga mazishi ya heshima kwa kipenzi chao, hapa kwetu mbwa wako akifa si haba kumtupa barabarani apondwepondwe na magari au kumtupia porini akaliwe na fisi.
 
Sijajua kama ni kisasi au ni laana ya mungu mpaka tumpate mshana Jr ,Tb Joshua Au pro Maji Marefu.....
Ni upuuzi tu, kila mja ana siku yake na ikitimia anaondoka haijalishi ni kichanga ama kikongwe
 
Back
Top Bottom