Watanzania na hofu ya wasilolijua

Watanzania na hofu ya wasilolijua

Burigi

Member
Joined
Jan 11, 2011
Posts
45
Reaction score
81
Wakati Chama cha Chadema wakifungua mkutano Wao wa uzinduzi wa kampeni ,Mheshimiwa Sumaye akihutubia mkutano huo alisema WATANZANIA wamekuwa wakitishwa na kudanganywa na kutawaliwa na hofu ya wasilolijua , usipotafakari maneno ya Sumaye unaweza uakayapuuza , lakini ukiyatafakari kwa mapana Utajua nini Sumaye anazungumza , ni ukweli usiopingika hofu ya tusilolijua ndio imekuwa mtaji wa Ccm kushinda uchaguzi mara zote na Sumaye mwenyewe alitumia mbinu hii Wakati akiwa ndani ya Ccm, kumbuka Sumaye alivyowatisha wafanya Biashara kipindi kile akiwaambia ili mambo yao yanyooke inabidi wachague CCM ..

Hii yote ni hofu ya usilolijua kwa hiyo bwana Sumaye anatakiwa kupongezwa kwa kufichua Siri hii ya Ushindi wa Ccm kwa miaka yote, Miongoni mwa Hofu usilolijua imeyotawala kwa miaka yote ni Ukichagua upinzani nchi itaingia vitani Kama Burundi na Rwanda, usichague upinzani hawana uzoefu etc ...

Leo hii hofu ya usilolijua watanzania wanaaminishwa kuwa wakifanya mabadiliko nchi itakuwa Kama Libya yote hii ni zile zile siasa za hofu ya usilolijua , Hofu ya usilolijua inaendelea kuonyesha fisadi mmoja asiepelekwa mahakamani , ambaye hatuonyeshwi Mali zake ni zipi na account zake zipo wapi na zina shilingi ngapi za wizi ni hatari kuliko mafisadi 1000 hiyo yote ni hofu ya usilolijua inayoendelezwa Miongoni mwa wananchi.

Swali langu ni moja hii hofu ya usilolijua itawachelewesha watanzania hadi lini kufanya maamuzi magumu juu ya nchi Yao? Naomba tuijadili hofu ya usilolijua na jinsi imevyochelewesha mabadiliko kwa miaka 20 sasa.
 
Mwaka huu tunaondoa hofu ya tusilolijua kwa kuchagua ukawa
 
Kweli kabisa..na hofu hii ya tusilolijua ndo ulofa wetu
 
UOGA WA USILOLIJUA ni mbinu ya kisaikolojia inayotumiwa na CCM miaka yote hii, ooh ukiwapa nchi wapinzani nchi itakuwa vita, ooh msiwape wapinzani urais, urais sio majaribio n.k
 
Back
Top Bottom