MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,229
- 50,379
Nimeona kauli za Watanzania wengi humu zinadhihirisha hawana uelewa wa nini maana ya maandamano. Kuna wengine baadhi yenu mnasema mpo radhi kutuazima mapanga, wengine tayari mnamuomba Magufuli aje atusaidie kupata suluhu ya vita. Hizo ni baadhi za kauli za kiajabu ajabu ninazoziona mkitoa. Yaani ni kama mumesubiri kwa hamu kama fisi kuona damu ikimwagika.
Naomba niwape darasa ya nini kinatendeka. Kuna baadhi ya Wakenya, nimesema baadhi maana utafiti umeonyesha sio wote ambao hawana imani na tume ya uchaguzi. Wanataka makamishna waondolewe na kuajiriwa wengine. Hii ni kutokana na sababu kadhaa walizoziorodhesha, kwamba katiba imeipa nguvu na uhuru tume ya uchaguzi, lakini viongozi wa sasa waliopo humo wanatuhumiwa kuegemea upande mmoja.
Ni kama zilivyo tume za uchaguzi za Tanzania, hususan ile ya Zanzibar ambayo ilidhihirisha kuwa na matatizo ya hali ya juu, lakini Watanzania wakaamua kulalamika kwenye mitandao kisha wakalala. Sasa Wakenya huwa kawaida hawalali kiulaini, lazima wajitokeze na kulalamika kwa maandamano. Haya ni maandamano dhidi ya serikali na sio vita vya wenyewe kwa wenyewe (civil war).
Tatizo ni pale, kuna Wakenya haswa wale wa kule Kisumu, Migori na maeneo hayo huwa wana mihemko ya kiaina. Huwa hawajui tofauti baina ya maandamano ya amani na yale ya vurugu za kawaida. Wanaishia kujipima ubabe wao wa kurusha mawe kwa kuwashambulia watu kwa mawe na kupora. Sasa hapo inakua hatari maana unapompiga polisi aliyejihami kwa bunduki, lazima utakua upo tayari kwa matokeo maana yule polisi ni binadamu na atahisi uchungu wa hilo jiwe lako. Halafu pia wazazi wa maeneo yale wanakua na upumbavu wa kiaina, wanaruhusu watoto kupitia pitia karibu na hizo vurugu.
Lakini kawaida katiba imeruhusu maandamano ya amani, kama ilivyotendeka Nairobi jana, wastaarabu waliandamana bila vurugu, wakalindwa na polisi na kuongozwa kwa njia salama na polisi wa trafiki kwa sababu ilikua haki yao ya kuandamana na kupinga wasichokitaka kwa mujibu wa katiba.