Watanzania maamuzi magumu nilazima ama tutaangamia

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,600
12,218
Ninavutiwa sana na kazi nzito na ngumu inafanywa na serikali ya Mh Dk Magufuli, chini ya mwavuli wa chama cha mapinduzi, chama tawala na chama mama Africa. Sitaki kubeza sera na mwelekeo wa chama chetu tawala ambacho kimepita changamoto nzito ktk kutufikisha hapa tulipo sasa. Kama taifa tunazo sababu zakumshukuru Mungu leo tupo hapa.

Ipo sababu yakila raia wa taifa hili kukaa chini nakuitazama serikali yetu ktk jicho la tofauti nakuangalia kule tumetoka na kule tunaelekea nakuyanyambuwa haya ktk jicho la tofauti. Watanzania tumekuwa kama watu tulio logwa ama kupumbazwa na aina ya mifumo ya maisha ktk serikali zetu. Unapo ingia kweye mtandao unakuta mtu kaandika maneno mengi akimkosoa Rais na tindo wakutumbuw majipu unatakiwa kuwa na kichwa cha mwendawazimu kumshawishi mtu kama huyu kuelewa nini maana ya utumbuwaji majipu.

Ndugu watanzania hili taifa linautajiri mkubwa sana ambao kama tusipojuwa jinsi yaku manage basi sio siri huko tuendako kunauwezekano mkubwa taifa hili tukagawana fito na mabati nakuacha maangamizi makubwa ambayo hayakuwahi tokea. Maamuzi mazito na magumu ambayo mh Rais anayachukua sasa yanaumiza wengi sana, yanadhoofisha nguvu ya watu kutumia pesa nakupoteza pesa mtaani. Lakini ukiangalia hili ktk macho yakisiasa unaweza ukasema Mh sasa anakwenda kuliangamiza taifa lakini ktk macho ya kesho yetu sivyo hivyo tunafikiri. ndugu zangu taifa hili kama tulikuwa hatujuwi lilikuwa limefika maali pabaya sana sana. Nimtu asie kuwa na mapenzi mema na taia hili ndie anaweza kulaani nakumuona Rais anachofanya sio sawa. Taifa hili ilifika mahali mtumishi mdogo sana ndani ya taasisi za serikali alikuwa akipiga rushwa ambayo hata Boss wake haoni ndani. Tulifika mahali kila mtu aliutikisa mti wa matunda yaanguke mabichi mauwa na alimradi yeye apate, hakuna cha mbunge wala mwenyekiti wakijiji wote walikuwa wakiipukutisha nchi kwa nafasi yake, si chama upinzani wala chama tawala wote wapukutishaji wa mti Tanzania.

Tunapo ona serikali inatumbua majipu haimanishi sasa maisha yatakuwa rahisi au ghali laahasha kile kinafanyika nikutengeneza uchumi ulio wa halisi ambapo kila mtu atawajibika kwa nafasi yake nakuvuna mapato ya halali pasipo kuibia nchi na wanyonge wa taifa hili. Ikiwa mtanzania wakule nyamagana ananunua bihashara ya maziwa ya kampuni Fulani isio lipa kodi ina maana anachangia pesa yake kwa mtu amabaye halipi kodi jambo lina mnyima fursa ya yeye kuja ifurahia kodi alio mchangia huyo mtu kuwa tajiri.

Maamuzi magumu kwa sasa ndani ya taifa hili ni sawa nakuchaguwa uhai ama mauti kwa hili taifa. uhai wa taifa hili unategemea sana uongozi huu wa sasa ama tutake au laa lazima majipu yatumbuliwe hata kamawengine miguno yao italeta aya za bible ama kuruhan ila uzima wetu kesho nikuhakikisha waujumu wa taifi hili wanatumbuliwa. tumechelewa sana shime Magufuli na ccm..
 
Mkuu kansa haitumbuliwi bila kuitoa kansa ccm Tanzania itakufa cha maana ni kufanya maamuzi magumu tuitoe kansa ili Tanzania ipone
 
Hizo ni siasa maji taka niambie nani utampa taifa ktk vyama wavijuwa wewe nenda Kenya uone maajabu na ukirudi tz utamshukuru Mungu
 
Hizo ni siasa maji taka niambie nani utampa taifa ktk vyama wavijuwa wewe nenda Kenya uone maajabu ukirudi tz utamshukuru Mungu
Kweli Tanzania tunamshukuru Mungu mnapora haki za wanzanzibar Na kufuta uchaguzi Na amani ipo ili ni la kumshukuru Mungu Na kudumisha amani maana kenya waliuana
 
Ninavutiwa sana na kazi nzito na ngumu inafanywa na serikali ya Mh Dk Magufuli, chini ya mwavuli wa chama cha mapinduzi, chama tawala na chama mama Africa. Sitaki kubeza sera na mwelekeo wa chama chetu tawala ambacho kimepita changamoto nzito ktk kutufikisha hapa tulipo sasa. Kama taifa tunazo sababu zakumshukuru Mungu leo tupo hapa.

Ipo sababu yakila raia wa taifa hili kukaa chini nakuitazama serikali yetu ktk jicho la tofauti nakuangalia kule tumetoka na kule tunaelekea nakuyanyambuwa haya ktk jicho la tofauti. Watanzania tumekuwa kama watu tulio logwa ama kupumbazwa na aina ya mifumo ya maisha ktk serikali zetu. Unapo ingia kweye mtandao unakuta mtu kaandika maneno mengi akimkosoa Rais na tindo wakutumbuw majipu unatakiwa kuwa na kichwa cha mwendawazimu kumshawishi mtu kama huyu kuelewa nini maana ya utumbuwaji majipu.

Ndugu watanzania hili taifa linautajiri mkubwa sana ambao kama tusipojuwa jinsi yaku manage basi sio siri huko tuendako kunauwezekano mkubwa taifa hili tukagawana fito na mabati nakuacha maangamizi makubwa ambayo hayakuwahi tokea. Maamuzi mazito na magumu ambayo mh Rais anayachukua sasa yanaumiza wengi sana, yanadhoofisha nguvu ya watu kutumia pesa nakupoteza pesa mtaani. Lakini ukiangalia hili ktk macho yakisiasa unaweza ukasema Mh sasa anakwenda kuliangamiza taifa lakini ktk macho ya kesho yetu sivyo hivyo tunafikiri. ndugu zangu taifa hili kama tulikuwa hatujuwi lilikuwa limefika maali pabaya sana sana. Nimtu asie kuwa na mapenzi mema na taia hili ndie anaweza kulaani nakumuona Rais anachofanya sio sawa. Taifa hili ilifika mahali mtumishi mdogo sana ndani ya taasisi za serikali alikuwa akipiga rushwa ambayo hata Boss wake haoni ndani. Tulifika mahali kila mtu aliutikisa mti wa matunda yaanguke mabichi mauwa na alimradi yeye apate, hakuna cha mbunge wala mwenyekiti wakijiji wote walikuwa wakiipukutisha nchi kwa nafasi yake, si chama upinzani wala chama tawala wote wapukutishaji wa mti Tanzania.

Tunapo ona serikali inatumbua majipu haimanishi sasa maisha yatakuwa rahisi au ghali laahasha kile kinafanyika nikutengeneza uchumi ulio wa halisi ambapo kila mtu atawajibika kwa nafasi yake nakuvuna mapato ya halali pasipo kuibia nchi na wanyonge wa taifa hili. Ikiwa mtanzania wakule nyamagana ananunua bihashara ya maziwa ya kampuni Fulani isio lipa kodi ina maana anachangia pesa yake kwa mtu amabaye halipi kodi jambo lina mnyima fursa ya yeye kuja ifurahia kodi alio mchangia huyo mtu kuwa tajiri.

Maamuzi magumu kwa sasa ndani ya taifa hili ni sawa nakuchaguwa uhai ama mauti kwa hili taifa. uhai wa taifa hili unategemea sana uongozi huu wa sasa ama tutake au laa lazima majipu yatumbuliwe hata kamawengine miguno yao italeta aya za bible ama kuruhan ila uzima wetu kesho nikuhakikisha waujumu wa taifi hili wanatumbuliwa. tumechelewa sana shime Magufuli na ccm..

Hii takataka ungeielekeza Lumumba labda ungeonewa huruma na kupewa angalau Kazi ya kufuta vumbi viatu vya wageni wanaolala KEBBY'S HOTEL.Kwa akili zako za kushikiwa zilizoathiriwa na ulaji wa viwavijeshi uliokithiri,unadhani sote tuna nakisi ya ubongo wa mbele kiasi cha kushindwa kufikiri sawa sawa .

Tangu tupate Uhuru Taifa hili limeongozwa na CCM pamoja na mtangulizi wake TANU.Hakuna aliyeizuia serikali ya CCM kutimiza wajibu wa msingi kwa Watanzania wa kuwaletea Maendeleo.
Leo hii unapotuletea hadithi za utumbuaji majipu as if majipu hayo yalizaliwa na kulelewa na chama kingine na sasa CCM imeamua kujipa Kazi ya kupambana nayo ili kuliondoa Taifa kwenye mkwamo wa Kiuchumi na umasikini uliotopea,unazifanya bongo zetu zipate kazi ya ziada ya kuutafakali uelewa wako.

Hata mje na lugha za mbinguni na sarakasi zenu za utumbuaji wa majipu,Ukweli ni kwamba mchawi wa Taifa hili ni CCM na serikali zake.Utovu wa maadili na kubebana kulikopitiliza kwa viongozi tuliowapa dhamana ya kuliongoza Taifa letu,ndiko kulikopelekea kuzaliwa kwa misamiati hii yenye lugha ya ukakasi masikioni mwetu iitwayo"kutumbua majipu"

Ugonjwa usipotibiwa kwa wakati hugeuka na kuwa sugu na kupelekea madhara makubwa kwa mgonjwa.Rushwa ndani ya Taifa letu ni kansa isiyoweza kutibiwa kwa ulaghai wa lugha za kisiasa za kutumbuana majipu.Wakati mnajinasibu kuwa dawa ya jipu ni kulitumbua,Watanzania wenye maono na Taifa lao tunaamini kuwa kwa hatua tuliyofikishwa na awamu zilizotangulia, mwili wa mama Tanzania umeshambuliwa vya kutosha na majipu,vipele,ukurutu na kila aina ya uchafu na kupelekea kuwa na kansa.

Kansa haiondolewi kwa kuitumbua,tiba ya kansa ni kukata sehemu ya mwili iliyoathirika ili kuizuia isisambae na kuudhuru mwili mzima.Suruhisho la kudumu la ubadhirifu na ufisadi hapa nchini ni kukiondoa madarakani chama kilichoulea na kuukuza ufisadi hapa nchini.Tiba ni kuung'oa mfumo wa kifisadi uliokomaa ambao umeng'ang'ania madarakani kwa zaidi ya nusu karne.

Kila siku tunahadaiwa na kelele za vibaraka wa mafisadi wakijifanya wanatumbua majipu,kumbe wanawaonea wanyonge wa Taifa hili kwa kuwatoa kafara watumishi wa Umma wakati mapapa ya ufisadi kila siku yanapishana katika Korido za Ikulu kwenda kujadiriana na "mtu wao" namna ya kuhakikisha analinda maslahi yao.

Yuko wapi mwenye uthubutu awezaye kusimama leo hii na kuzileta mezani kashfa zote za ufisadi zilizolitafuna Taifa?Au Kitendo cha watumishi wa Umma kuchelewa kuripoti kazini ndiyo ufisadi pekee unaolitafuna Taifa letu?

Mtumbua majipu anasemaje kuhusu mtangulizi wake aliyepora Mali ya Umma na kujimilikisha yeye na familia yake?Kuna ufisadi zaidi ya Rais kujigeuza mjasiliamali na kufungua kampuni yake binafsi kwa anuani ya Ikulu?

Huyo mtumbua majipu wako anasemaje kuhusu uuzwaji kiholela wa nyumba za serikali?Anasemaje kuhusu EPA,KAGODA,DEEPGREEN,ESCROW,RADA,MABEHEWA FEKI na RICHMOND?Mbona amekuwa kimya katika hayo kana kwamba hayajaathiri kwa namna yoyote uchumi wa Taifa hili?

Kuendelea kugeuzwa manamba wa kukaririshwa kaulimbiu za "hapa Kazi tu" wakati vijana wasomi wa Taifa hili hawana Kazi kutokana na CCM kuuwa viwanda ambavyo vingewaajiri ni utaahira usiovumilika.

Hatuhitaji maigizo na mazingaombwe ya ziara za kustukiza,tunahitaji Mipango na mikakati thabiti ya kumkomboa mwananchi wa kawaida ambaye amegeuzwa daraja la mafanikio ya wachache,aonje neema tulizojaaliwa na Mungu ili naye ajivunie kuwa Mtanzania.
 
Ase gombea ubunge JF, kura yangu umeipata
 
Mkuu kansa haitumbuliwi bila kuitoa kansa ccm Tanzania itakufa cha maana ni kufanya maamuzi magumu tuitoe kansa ili Tanzania ipone
We vipi? Tumia akili kidogo. Kansa haiwezi kuitoa kansa. Eti ccm 'B' iitoe ccm 'A', thubutu. Isingekuwa gia ya angani labda.
 
Wewe ndio utumie ajili sijataja chama cha siasa chama chochote cha siasa ata chauma, cuf, chadema, tlp vikiweza kuiondoa huu mfumo toka enzi za ukoloni tutaikomboa Tanzania
 
Back
Top Bottom