Watanzania kuna kitu wanataka kumwambia Tundu Lissu

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
17,115
42,640
Hatimaye Tundu Antipasi Lissu Amerejea Nyumbani:

Mheshimiwa sana, Mzalendo wa Kweli, Mwenye Upendo wa Kweli, Tundu Antipasi Lisu karibu nyumbani Tanzania. Tanzania, nchi ambayo kama siyo kwa mapenzi ya Mungu usingeweza kuiona tena kwa macho ya mwili.

Tundu Antipasi Lisu Dhihirisho la Ushindi wa Mungu

Tundu Antipas Lissu, kuishi kwako mpaka leo siyo ushindi wako bali ni ushindi wa Mungu dhidi ya shetani. Baada ya Mungu kumshinda shetani, na ukuu wake hudhihirika, wewe uliyelala mauti na Mungu, na Mungu kuyashinda mauti ya shetani, itakuwa ni laana kwako nasi tunaosimama na Mungu wa haki, siku moja tukarudi tukaungana na shetani. Tukifanya hivyo, ushindi wa Mungu dhidi ya shetani hautakuwa na maana

Tundu Antipas Lissu ni Mageuzi ya Falsafa ya Siasa za Tanzania

Siasa za Tanzania zimejaa ulaghai, hila, unafiki, uoga, rushwa na hata ushirikina. Lakini siasa ndiyo hutoa wafalme, watawala na viongozi wote Duniani. Je, ni halali anayewaongoza watu kuwa mnafiki, mlaghai, mwongo na mtoa rushwa? Hapana. Siyo sahihi. Imekuwa kama ilivyo kwa sababu katika siasa za Tanzania ndiko shetani anakoishi.

Tundu Lisu unatakiwa kuzigeuza siasa za Tanzania kutoka kwenye hali ya sasa mpaka kuifanya siasa kuwa ni ukweli, uungwana, ujasiri wa kuunena ukweli na usafi dhidi ya kila uchafu ufananao na rushwa. Leo kwenye kura za maoni ndani ya CCM ni kilio. Kwa sababu kila aina ya uchafu vimetumika. Iwe ni wapinzani au CCM, wamechoka siasa za uwongo, unafiki, hila na uoga. Wewe ndiye utayaongoza mabadiliko haya.

Tundu Antipasi Lissu ni Kifutio cha Dhulma na Upendeleo

Tanzania ya leo, watu wanalia kwa uonevu, chuki na upendeleo. Watu wanalalamikia upendeleo wa ukanda, undugu, na kwa mbali udini. Watu wanalia kwa kudhulumiwa mali zao walizositafuta kwa haki. Watu wanalia kwa kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi bila ya kuhujumu uchumi, kutakatisha fedha bila ya kuwa na hela za kutakatisha. Lakini kosa lao kubwa ni ama hawasifu juhudi, au wanakosoa juhudi au hawalambi nyayo za watawala.

Wewe ndiye sauti yao, wewe ndiye mkombozi uliyetumwa kwaajili ya wote. Wanaohitaji msaada wako siyo CHADEMA, ACT, au wapinzani tu, lakini wapo wengi ndani ya CCM pia. Wanalazimika kusifu mpaka kufikia kukufuru. Wengine mpaka wanafikia kumwita mwanadamu mwenzao ni Yesu Kristo (kufuru kubwa!). Hawa wote hawafanyi hivyo kwa kupenda bali kwa sababu ya hofu. Wamekuwa na hofu na uoga wa kupitiliza. Hawa wanahitaji msaada wako zaidi kuliko wafuasi wa vyama vya upinzani.

Tundu Antipas Lissu Umeshindishwa ili Umshinde Shetani, Siyo CCM.

Adui wa Watanzania siyo wanaCCM, siyo CCM wala siyo viongozi wa CCM bali ni Shetani aishiye ndani ya CCM. Ukisoma falsafa ya CCM na ya mwasisi wa CCM ipo wazi sana, ni kuheshimu utu na uhai wa binadamu, kulinda uhuru wa raia, kuheshimu uhuru wa maoni LAKINI lakini CCM ya leo inaua, inatesa, inapoteza watu, inajeruhi, inaonea, inapendelea na kubagua. Haya siyo ya CCM bali ni shetani aishiye ndani ya CCM. Mh. Tundu Lisu unganisha Watanzania wote wenye dhamira njema bila ya kujali vyama vyao, makabila yao, kanda zao, dini zao au tofauti zingine zozote ziwazo.

Tundu Lisu Antipasi Lissu Ishara ya Amani

Amani ya kweli ni tunda la haki, usawa na ukweli. Shetani haishi CCM tu bali kwa yeyote mwenye kumkaribisha. Popote uwapo tetea na usimamie haki maana huo ndio ushindi wa Mungu aliopenda audhihirishe kwako.

Mkono wa Bwana Ukasimame nawe popote, na ghadhabu ya Mshindi Mkuu ikawe juu ya Wenye kuikanyaga Haki.
 
Yes, sio tu watanzania wanataka kusema wamechoshwa na utawala uliopo chini ya serikali ya CCM, lakini pia wameonesha kwa vitendo ni jinsi gani walivyo wastaarabu, pale wakiachwa wafanye mambo yao kwa uhuru bila kusumbuliwa na jeshi la polisi.
 
Mafisadi mpaka sasa wanajinyea huko walipo. Leo wameogopa hata kuleta mapolisi yao kutisha watu maana zile barua walizo tumiwa kila mtu yupo chumbani anajisomea asije akaitwa kule Uholanzi mamaye zao.

Leo tumetembea kwa raha kabisa hapa mjini bila bugza za hawa wakoloni weusi. Yaani unajenga eti barabara kwa kodi zetu halafu Unataka tukuimbie nyimbo za kukusifu pia umwage damu zetu bila hatia.
 
Mafisadi mpaka sasa wanajinyea huko walipo. Leo wameogopa hata kuleta mapolisi yao kutisha watu maana zile barua walizo tumiwa kila mtu yupo chumbani anajisomea asije akaitwa kule Uholanzi mamaye zao.

Leo tumetembea kwa raha kabisa hapa mjini bila bugza za hawa wakoloni weusi. Yaani unajenga eti barabara kwa kodi zetu halafu Unataka tukuimbie nyimbo za kukusifu pia umwage damu zetu bila hatia.
Kwa hiyo leo mmeogopwa?
 
Umeandika madini matupu kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Hongera sana.
WAZO MBADALA!! Hivi nyie ma GT hamjui Huyu mtu alienda ACT ni kazi maalum, watu hawajui kuwa kaja upinzani kugawa kura za wapinzani. Katumia janja ya kujitwika uhasama kumbe hamna lolote. Hata JPM anajua hilo ndo mana hawamsumbui
 
sera ya ccm ya magufuli ni rushwa na ubabe. tutaenda jino kwa jino mpaka waiache nchi yetu hawa malofa.
 
Back
Top Bottom