Watanzania kamwe tusikubali siasa za chuki na uchochezi wa wanasiasa

Rich Hash

Senior Member
Mar 7, 2017
149
203
Siasa ya Tanzania kwa sasa imekuwa ni ya chuki baina ya upinzani dhidi ya serikali. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Raisi Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa ikikumbana na vikwazo vya kila namna ili kuiyumbisha serikali. Hii yote ni matokeo ya kile ambacho wengi hawakutegemea kukiona katika nchi hii. Vita imekuwa ni kubwa sana kwani maslahi ya wachache yaliyosababisha Tanzania tukazidi kuwa nyuma yameguswa kwa kiasi kikubwa. Mianya ya rushwa imezibwa kila kona, ufisadi unadhibitiwa kila sekta, mianya ya madawa ya kulevya imedhibitiwa, uwekezaji mkubwa unaonekana ukianza kushamiri siku hadi siku kupitia mikataba ambayo nchi inaingia na nchi marafiki na Tanzania, kukua kwa uchumi kwa kasi zaidi na uboreshaji wa miundombinu ya kijamii(afya, elimu), usafiri wa barabara(mwendokasi na flyovers), reli(Standard Gauge Railway), anga(Ndege mpya) na maji.

Ukifikiria kwa undani basi utayaelewa yale maneno ya wahenga yasemayo, mti wenye matunda ni lazima upigwe mawe. Wapiga dili wamekosa njia rahisi za kuiangusha Tanzania na sasa kimbilio lao limekuwa kwenye siasa ili kuwaaminisha Watanzania kuwa serikali haifanyi chochote. Fanya upembuzi yakinifu wa yale wanayoyapigania kama kweli wanayatekeleza na kutoka mioyoni mwao au ni janjajanja tu?
  • Iko wapi vita ya ufisadi ukiwa umekumbatia mafisadi papa ndani ya chama chako?
  • Iko wapi demokrasia ya kweli ikiwa hakuna demokrasia ndani ya chama chako?
  • Ni lini utafanyika uchaguzi wa wenyeviti wapya wa vyama vyenu? Au waliandikiwa uenyekiti wa maisha?
  • Ni kanuni zipi mlizozitumia kumpitisha mgombea wenu Edward Luwassa kuwania uraisi kupitia Chadema na Ukawa 2015?
  • Je, kuwalipa fadhila Wenje(Kukosa ubunge) na Masha(kwa kumuachia uraisi Tundu Lissu TLS) kwa kuwapa tiketi ya kuingia EALA kwa maamuzi ya viongozi wenu ndio Demokrasia ya kweli?
GO ON RAISI WETU JOHN POMBE MAGUFULI, HII NDIYO TANZANIA MPYA TUITAKAYO
nape nnauye.PNG
 
View attachment 500929
Jibu ni kuwa wakati wale walipokuwa CCM hatukusikia upinzani wa aina hii,ila tu baada ya wale kukatwa na kushindwa kwenye uchaguzi na kukimbilia upande wapili wamekuwa wakiendesha vita vya kuihujumu serikali,hawa wana tabia za hovyo na hatushangai sababu hata walipokuwa CCM walifanya kila hila wapitishwe,walimwaga fedha makanisani na misikitini,walimwaga fedha kwa wajumbe wa vikao mbalimbali,walileta mafuriko hewa,kwa hiyo bado hawakosi kufanya hujuma huko waliko,lakini Mungu ni mkubwa mbinu zao zinajulikana kwa hiyo wanajisumbua tu,tutaonana kwenye debe 2020.tuta wa-kata.
 
Watanzania wanaishia ktk umasikini ulio topea
Wajinga wanazidi kuongezeka kwa kukosa elimu
Matibabu duni yasiyokidhi afya
Udikiteta na utekaji kuongezeka na dhuruma kwa wananchi wanyonge inaongezeka
Vilio kila mahali.
Huyu mtu hatufai wananchi ongezeni chuki dhidi ya serikali yake
 
Tatizo watanzania kila kitu tunajifanya wajuaji! Tutaendelea kuwa masikini mpaka pale amavyo tutaamua kusimamia ukweli!
 
Mungu yuko pamoja nasi na atatufikisha tu.

Nitamchagua tena JPM 2020 na akimaliza tubadili katiba aendelee.
 
Wakati mwingine unaweza usione wala kuhisi kuwa kuna uchafu sehemu ulipo hadi utoke! Wanaotoka ccm wanapata kuelewa ugumu wa kubadili mfumo baada ya kujiengua.
 
Back
Top Bottom