Watanzania hebu tufikirie maneno mazito na ya mwisho kutoka kwa Hayati Mwalimu Nyerere kabla hajafariki dunia

Watanzania hebu tufikirie maneno mazito na ya mwisho kutoka kwa Hayati Mwalimu Nyerere kabla hajafariki dunia

Rijali jandoni

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2018
Posts
2,165
Reaction score
2,251
"Najua nitakufa sitapona ugonjwa huu nawaacha watanzania wangu najua watalia sana nami nitawaombea kwa Mungu, naondoka nikiwa nime waachia taifa moja lenye umoja na amani. Wosia wangu kwao waipende nchi yao kama wanavyo penda mama zao, wajue hawana nchi nyingine zaidi ya Tanzania" Mwisho wa maneno ya baba wa Taifa na akafariki.

Katika nchi zote za Africa naweza diriki kusema hakuna taifa lenye watu wazalendo, upendo na imani juu ya taifa lao kama watanzania.

Umoja huu na upendo tulio nao juu ya ardhi hii, si kwasababu ni waoga ila tumekuzwa katika misingi ya umoja, ushirikiano na upendo baina yetu na nchi yetu kwa ujumla.

Wenye ridhaa katika nafasi tofauti ndani na nnje ya Tanzania tambueni hamna nchi nyingine ispokuwa Tanzania, kwenye amani Tanzania ni mtoto tumlinde kwenye shida na mateso Tanzania ni mama tutamlilia..

Kwa namna hii viongozi kwa wananchi haina haja ya kusahau kuijenga nchi yetu kwa upendo maana haileti amani pale ambapo kila kitu kuhusu mradi au tenda kinatoka lakini hakuna utekelezaji inafika wakati hata kukaa na kutembelea maeneo ya nchi inatupa wasiwasi kwa sababu ya miundombinu isio malizika, na huduma nyingine ambazo hazija fanyika kabisa ila ni ahadi na paper works kutoka kwa viongozi wenye weledi usio tosha.

Wewe kama kiongozi wa ngazi fulani mbunge, waziri, mkurugenzi hata mtendaji barabara unayo acha kwenye vumbi na matope kesho utapita hapo ina maana gani na italeta hisia zipi kama umepokea hela na huku fanikisha mradi husika?

Kwenye hospitali au kituo cha afya ulicho omba na kukabidhiwa hela ukala kesho kuna jamaa na ndugu zako watakosa huduma na kufariki hapo je utakuwa na amani baada ya haya yote?

Vivyo hivyo miradi ya shule ni mingapi haija kamilika kwa sababu hela hazijafika eneo husika? mataifa yote tunayo ona huko nnje yana ustaarabu, maendeleo, usafii na amani kama tulio nayo kwasababu wananchi wao wamepewa mazingira mazuri juu ya elimu zote za darasani na kijamii, Tanzania tunajitahidi ila kwa kasi ya dunia ya sasa bado tunahitajika kuendelea zaidi.

Kwenye mazingira ya biashara ni eneo zito ila tuwape na tuwalinde wawekezaji wa ndani na wafanya biashara naelewa ni ngumu kuanzisha viwanda vikubwa kwa sababu ya sera na mikataba ya mataifa makubwa juu ya nchi za africa, lakini basi hata kwa vitu vinavyo ingia tuvifikirie kwenye utaratibu wake wa kuingizwa nchini ili vilete unafuu au vichache vizalishwe ndani hiyo nayo itakuwa upendo kwa taifa lako

Hatusemi kwamba hakuna viongozi watendaji hapana wapo japo tunahitaji uwajibikaji halisi juu ya nchi na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa kipindi hiki na vingine vinavyokuja mifumo na taasisi husika zitengeneze na kuleta watendaji wenye nia ya kweli juu ya nchi, nafasi zikaliwe na watu weledi na wenye ujuzi wa eneo husika ili kuleta utendaji bora na wenye ufanisi

Nafasi wasipewe watu sababu ya ubini, ujamaa au undugu tutaweza zorotesha Tanzania yetu, kwa miaka 75 maximum ya Uhuru tunatamani kusiwepo na shida ya umeme, maji, barabara, uhaba wa shule itakuwa ni huzuni na aibu kwetu sisi watanzania kama bado haya mambo yataitesa hii nchi

Tunaelewa nafasi na majukumu ya uongozi ni magumu sana mnakutana na changamoto nyingi kwenye mikataba na mambo mengine tuna tambua dunia ya huko nje haina huruma japo hawapendi wananchi wajue hilo, mnajitahidi lakini tunahitaji utendaji mkubwa zaidi maana uwezo tunao wa kuyafanya yote haya ila tutangulize upendo na utanzania kwenye kila fursa tunazo pata tusifikirie kwa ubinafsi bali tuweke kila kitu kwa maslahi mapana ya Taifa

Tukiwa na hospitali nzuri na mfumo wa elimu tuka uongezea vitendo zaidi, waziri atatibiwa hapo hakuna haja ya kwenda nnje, mbunge vivyo hivyo polisi wataenda pia wao na familia zao wakulima wafugaji na wafanya biashara wote watafika hapo tuipende Tanzania

Nchi ijengwe kwanza ndio watu waanze kula matunda mataifa mengi ya huko ndio yafanyavyo Singapore, Malaysia, China, Korea na Japan viongozi wanakula matunda ya utendaji wao baada ya ujenzi ila kwetu kwanini ni ngumu?

Mungu awalinde niwatakie majukumu mema.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Njiti Moja ya kibiriti huchoma msitu Mkubwa

Hiyo njiti ithibitiwe haraka sana

Chama kilie na mtu mwenye njiti hiyo hakikisheni hili halitokei!!

Kuna Chama kilimgundua mshika njiti ni mjanjamjanja kikampora njiti
Na aliye mpora alitumia timing Kali sana(ukweli ni Mungu alisaidia)

MUNGU aingilie kati njiti ilowe isiweze lipuka!!
 
Babu bul hiyo njiti imefichwa?, kama ipo ime hifadhiwa wapi na nani?
 
Angekuwa yupo makini asingeandika katiba ya kihuni na mifumo mibovu huyo jamaa hakuwa na maono Makubwa but he did what he did RIP
Nadhani kwa ule muda Mwalimu alijua kabisa kwa nyakati zile palikuwa hakuna chama chenye nguvu na ushawishi kama Chama Cha Mapinduzi lakini kuja kwa vuguvugu la vyama vingi bado ilikuwa na ukakasi maana ni ngumu kuamini mfumo ulio pendekezwa na watu walio kuwa wanatamani mengi kutoka kwetu

Na uzuri zaidi Mwalimu aliweza kukiri makosa, kuna baadhi ya nyadhfa wakipata watu wenye weledi, itikadi ama akili fulani basi wataweza tumia vibaya haya yote aliona mamlaka na nguvu walio ipendekeza kwenye taasisi na vyama fulani na huenda lilikuwa na faida kwa wakati ule

ila kutokana na mabadiliko ya siasa na mifumo mbali mbali haina budi mambo fulani kuonekana kama disadvantages baada ya kipindi fulani.

Hoja nzito ilio ibuka kwangu sasa hivi je mabadiliko yanayo hitajika na watu fulani yatafanyika kwa uzalendo huku yakizingatia maslahi mapana ya taifa?

Tusije badili vifungu vitakavyo tikisa misingi ya taifa ambayo yote yanabebwa na amani

Au una onaje hili
 
Nadhani kwa ule muda Mwalimu alijua kabisa kwa nyakatibzile palikuwa hakuna chama chenye nguvu na ushawishi kama Chama Cha Mapinduzi lakini kuja kwa vuguvugu la vyama vingi huenda bado ilikuwa na ukakasi maana ni ngumu kuamini mfumo ulio pendekezwa na watu walio kuwa wanatamani ulivyo navyo

Na uzuri zaidi Mwalimu aliweza kukiri makosa, kuna baadhi ya nyadhfa wakipata watu wenye weledi, itikadi ama akili fulani basi wataweza tumia vibaya haya yote aliona mamlaka na nguvu walio ipendekeza kwenye taasisi na vyama fulani na huenda lilikuwa na faida kwa wakati ule

ila kutokana na mabadiliko ya siasa na mifumo mbali mbali haina budi mambo fulani kuonekana kama disadvantages baada ya kipindi fulani.

Hoja nzito inayo ibuka je manbadiliko yanayo hitajika yatafanyika kwa uzalendo huku yakizingatia maslahi mapana ya taifa?

Tusije badili vifungu vitakavyo tikisa misingi ya taifa ambayo yote inabebwa na amani

Au una onaje hili
Mnamkuza Sana huyo Mwalimu kwa wakati ule wakati gani

Katikba imekuwa formed 1977 unataka kunambia mwaka 1977 ni mbali.

Mnabidi kukubali kuwa Nyerere alifanya Kazi nzuri Ila alikuwa hana maono na alikuwa selfish.
 
Kinacho tokea hapa nadhani baadhi ya watu wanashindwa elewa nini alicho fanya mwalimu na kutaka kumbebesha mambo mengine ambayo yalipaswa yafanyike currently,Mwalimu hajakuzwa yeye aliweka misingi ya taifa, nikiwa na maana Tanzania ilianza kujengwa kwa umoja kutokea 1961 maana kabla ya hapo juhudi za kuunganisha makabila na kaya zote nchini ili ziwe na njia moja kama watu wamoja.

Kwa namna hiyo Mwalimu nyerere aliweka msingi wa uundwaji wa taifa la Tanzania akiwa na malengo fulani ndio maana unakuta baadhi ya miradi wana reflect kwa kusema ilikuwa ni ndoto ya Mwalimu nyerere.
 
Mnamkuza Sana huyo Mwalimu kwa wakati ule wakati gani

Katikba imekuwa formed 1977 unataka kunambia mwaka 1977 ni mbali.

Mnabidi kukubali kuwa Nyerere alifanya Kazi nzuri Ila alikuwa hana maono na alikuwa selfish.
Tukija swala la 1977 kwa uhalisia sio mwaka wa mbali sana ila mwenye maendeleo ya taifa na watu wake bado hatukuwa na watu weledi kutokana na idadi na maendeleo machache kwa wakati ule.

Kwa nchi nyingi zilizokuwa na rasilimali watu na tuliweza kuaminishwa kuwa tupo sawa kiuchumi waliweza kutupiku sababu ya idadi ya watu kwa mwaka ule na hata kama hawakuwa na elimu ya kutosha ila walipo ipata waliweza kuwa taifa jingine kabisa angalia nchi kama Thailand, singapore, korea na kuendelea.
 
Haya ndo mambo yanayowafanya watanzania kuwa wajinga .

Yaani mwaka 1977 unasema ni mbali?

Kuwa serious na unachoongea

Je kama alikosea kuandaa katiba mwaka 1977 alishindwa vipi kumuomba Mwinyi au mkapa kufanya amendments ya katiba since 1977-1995?

Mimi nachukia watu wanafiki na wajinga ambao hufanya mambo kiubinafsi .

I hate them .
 
Mnamkuza Sana huyo Mwalimu kwa wakati ule wakati gani

Katikba imekuwa formed 1977 unataka kunambia mwaka 1977 ni mbali.

Mnabidi kukubali kuwa Nyerere alifanya Kazi nzuri Ila alikuwa hana maono na alikuwa selfish.
Hoja ya mwisho ni kweli kazi aliifanya ila kwa muda wake aliweka misingi yeye aliwapa watu ndoto na muelekeo ila hakukuwa na barabara ilio kamilika

Kwa lugha nyingine yeye alitoa structural direction ya baadhi ya mambo, wa kulaumiwa kuhusu utekelezwaji wa maono nadhani ni baada yake na huenda ni kweli dira ya muda mrefu ilikosekana pia kutokana na ukosefu uahaba wa watu wajuzi kwenye taifa
 
Ukiachana na kukopi na kupesti sioni alichofanya tofauti na kupambania harakati za Uhuru .

Kiongozi mwenye akili huwa anakuwa sio mbinafsi .

"Eti matokeo ya rais yakitangazwa hayarusiwi kuhojiwa sehemu yoyote"

According to katiba alikuwa anaandaa katiba inayomuhakikishia madaraka na ulaji
 
Huu ni urongo hakunaa hakunaa
Nyerere hakusema chochote alivofika London alizima maxima hakuongea Tena
Acheni kutudanganya kijingajinga hapa nchi inaendeshwa kwa porojo
 
Haya ndo mambo yanayowafanya watanzania kuwa wajinga .

Yaani mwaka 1977 unasema ni mbali?

Kuwa serious na unachoongea

Je kama alikosea kuandaa katiba mwaka 1977 alishindwa vipi kumuomba Mwinyi au mkapa kufanya amendments ya katiba since 1977-1995?

Mimi nachukia watu wanafiki na wajinga ambao hufanya mambo kiubinafsi .

I hate them .
Si mwaka wa mbali lakini tukija swala la maendeleo ya nchi tunatakiwa tujipime kwa huo mwaka 1977 tulikuwa na nini, na kipi tulichokuwa nacho tungeweza kuendeleza taifa, nimegusia kwa kusema tulikosa rasilimali watu, na nyongeza zaidi taifa halikuwa na wabobezi ndio maana baadhi ya sekta bado tulitegemea watu wa nnje sababu ya ukosefu wa watu na hata viwango vya elimu zao

Nchi yoyote duniani inakuwa kwa idadi kubwa ya watu ila wawe walio na misngi mizuri ya maendeleo yaani walio elimika, wenye afya njema na watulivu

Haya bado tuna pungukiwa

Swala la katika na mchakato wa vyama vingi 1992 tukiri wazi tuliweza kupokea sera hii sababu ya mdororo wa kiuchumi tuliokuwa tuna upitia taifa halikuwa tayari kwenda kwenye multipartism

Na issue nyingine hata kwenye mfumo huo hakuna kuaminiana

Issue ni weledi wa viongozi wa pande zote juu ya maslahi mapana ya taifa, yaani hata kama mtu anatokea Chadema, Cuf, Nccr ama Ccm wawe watu weledi wenye vigezo vyote vya uongozi

Sio kama sasa tunaweka mpaka class seven hata barua hajui kuandika na wengine wamefeli hata vyeti hawana hii ndio ninacho maanisha tuna hitaji watu weledi ili taifa lisonge mbele na wenye uchungu wa nchi hii
 
Pamoja na mazuri yake Nyerere ni wa kumlaumu kwa kutuachia katiba tuliyo nayo na kwa kuua vyama vingi alipoingia madarakani na TANU yake
Huenda ni kweli ila vyama vingi vya mikoani nadhani havikuuliwa moja kwa moja ila walishawishi kuunda chama kimoja kitakachokuwa na ushawishi upande wa Tanganyika kabla ya kwenda kuungana na Zanzibar

Nchi hii ingekuwa kwenye ukabila na kuto kuunganisha huenda tungeweza kuwa kama south africa, lesotho na botswana hawa ni jamii moja ila ilikuwa ngumu kuwaunga
 
Back
Top Bottom