Hakika watanzania wenzangu tuamke kwa maslahi ya watanzania wenzetu hususani wale wasiojua kusoma na kuandika, watoto wadogo, wazee na wote wasio na mamlaka katika nchi. Hivi ni Nani aliyewaloga wasomi wetu? Hivi ni kweli nchi INA wasomi na wataalam?
Leo napenda niongelee jambo moja tu ambalo linahusu mchakato wa Kura ya maoni. Ni hivi majuzi tumesikia kuwa mwenyekiti wa tume ya katiba ameahirisha siku ya uchaguzi wa kura ya maoni kwa mda usiojulikana.
Jambo kubwa hapo ni kuwa imeshindikana kuwaandikisha watanzania wote kwenye daftari LA wapiga kura. Hapo ndipo nataka kuwauliza watanzania wenzetu wale wasomi na wana zuoni. Ni mtanzania yupi ambaye atakuwa na haki ya kupata kitambulisho cha uraia ambaye hana sifa za kupiga kura?aidha ni mtanzania yupi ambaye anasifa yakupiga kura na asiwe na sifa yakuwa RAIA? Kwanini tusiwe na kitambulisho kimoja tu cha uraia ambacho kitaainisha taarifa zote?katika kitambulisho hicho kitaainisha habari zote zinazomuhusu muhusika hata kama atakuwa na upungufu wa akili.
Kama taasisi muhim zitaunganishwa wakati wa kuzaliwa hakutakuwa na usumbufu hata wakati wa kupewa kitambulisho kwakuwa taarifa zote zitakuwa wazi. Amakweli asiyesikia LA mkuu huvunjika mguu.
Bado naona tatizo lipo pale pale tulipoliacha azimio LA arusha.kinacho angaliwa hapo ni maslahi binafsi katika hizo tenda za vitambulisho.
Hatujachelewa, tukitaka kufanikiwa tulirejee azimio letu LA Arusha. Mtumishi wa umma asiwe mfanyabiashara. Migomo na maamuzi yote yanayotolewa bila kufanya utafiti chanzo chake ni ukiukwaji wa maadili ambao umeainishwa kwenye azimio la Arusha.
Amkeni Watanzania!