py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,476
- 4,447
Baada ya msimu wa 2016/2017 kuisha kwa klabu ya Azam kufanya vibaya mfululizo kwenye ligi wameamua kufanya overhauling ya management na wachezaji na tayari CEO Said kawemba ametumbuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Abdul Mohamed na baadhi ya wachezaji wametemwa akiwemo John Bocco Adebayor.
Wiki mbili sasa watangazaji wa vipindi vya michezo wamekuwa wakiitupia lawama Uongozi wa Azam kwa kitendo cha kumwacha Bocco atafute pasture sehemu nyingine na wengine wakisema Bocco hapaswi kuchezea klabu tofauti na ya Azam hapa nchini sababu Bocco ni moja ya wachezaji walioifanyia makubwa Azam.Wapo wanaosema Bocco ni nembo ya ya Azam na wapo waliothubutu kusema Bocco abakizwe akae tu na apangiwe kazi nyingine
Klabu ya Azam ilianza kupotea na kufa walipoanza kuleta siasa zao kama vilabu vya yanga na simba.
Tusisahau ni juzi tu makocha raia wa Hispania walimkata Bocco na kuwaambia viongozi kuwa Bocco hayupo kwenye mipango yao kwasababu walizotoa wao lakini viongozi wa Azam wakiwapigia magoti makocha wale na kuwasihi kwa heshima na jina la Bocco afanyiwe fair abakishwe.
Tukio la pili ni makocha wapya "wazungu waliokuja sasa kwenye ripoti zao wamesema hawana mipango na wachezaji kadhaa na Bocco akiwepo ,ni coincidence makocha tofauti wanaokuja wanakukata jina lako na wanasema haupo kwenye mipango yao kwahili Azam wamecheza kama pele sababu maamuzi ya kocha yaheshimiwe ,umemuajiri mwalim kwa pesa ndefu maamuzi yao yasiingiliwe wawe huru,kama Mara ya pili uongozi wa Azam wangewapigia goti makocha kuwasihi wambebe Bocco ningewaona wapuuzi.
Hoja ya kusema Bocco ni legend aachwe japo hayupo kwenye mipango ya kocha ni ujinga au abakishwe klabuni acheze mechi moja moja kisa ni mkongwe na alifanya mazuri .
Raul Gonzalez Blanco alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Real Madrid lakini alivyokatwa na mwalimu sababu ya kiwango cha kutoweza kushindana aliondoka zake na kwenda schalke 04
Iker Casillas kipa bora kuwahi kutokea Real Madrid baada ya kiwango kushuka akawa anawekwa bench na mchezaji mkongwe anapowekwa benchi kiburi humuanza akatupwa zake Porto .
Xavi Hernandez Maestro Mara baada ya kuona atakuwa na dakika chache za kucheza sababu kocha option yake ni Rakitic alisoma alama za nyakati mapema akasepa
Azam imekuwa mbovu licha ya uwekezaji mkubwa ni sababu ya management mbovu na kuwakumbatia amateur players .Napongeza kwa uamuzi uliofanya ya kusuka management na kikosi ,
Mussa mgosi alitupwa mtibwa saizi ana cheo Simba
Bocco Kama mchezaji atataka apate dakika za kutosha na makocha wamesema hayupo kwenye mipango yao sasa endapo akibakishwa alipwe mshahara na akae bench hata yeye hatofurahia
Pep alipochukua Barcelona aliwakata akina Gaucho ,Deco ,edmilson ,Yaya Toure ,Eto'o ,Marquez nk na uongozi wa timu iliheshimu matakwa ya kocha.
Mchezo pekee wenye uhakika 100% wa kucheza sehemu moja ni Golf
Akina Phillip Lahm kustaafia timu hiyo hiyo sio kwa upendeleo bali kwa ufanisi na uwekedi wao.
Bocco ndio mpira ulivyo fanya bidii piga kazi simba ukistaafu utarudishwa ufanye kazi kama kali ongala
Lakini ukiendelea na u-slow wako ,uvivu uwanjani utayaoga matusi ya mashabiki wa simba ohoo simba sio Azam utaiona dunia chungu ,jikaze zaidi huko
Mwisho nchi hii kuna watangazaji na wanaojita wachambuzi "mabashite" kuna station moja walisema eti apangiwe kazi nyingine nilibaki mdomo wazi sasa mchezaji apangiwe kazi gani kwani ile siasa ukitumbuliwa ukurugenzi unapewa ukuu wa wilaya ???