Wataalamu wa Magonjwa ya Akili wadai Rais Donald Trump Ana Matatizo ya Akili.

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Kikundi cha madaktari wa ugonjwa wa akili waliokutana katika kikao cha dharura huko Yale University Marekani wamedai kuwa Rais wa Marekani Donald Trump ana matatizo ya kiakili (dangerous mental illiness) na hafai kuongoza nchi hiyo. Akinukuliwa kwa kusema Dr. John Gartner wa Yale's School of Medicine in New Haven, Connecticut kuwa Donald Trump kuendelea kuwa Rais Marekani ni hatari kubwa kwa usalama wa taifa hilo kubwa duniani.
Rais Donald Trump alidai kuwa mahudhurio ya watu katika siku alipoapishwa kuwa watu waliohudhuria walikuwa ni wengi kushinda wakati Barrack Obama alipoapishwa ambapo madai hayo ni ya uongo. Rais Donald Trump majuzi aliamuru Bomu lenye uzito wa tano 10 litumike huko Afghastan hiyo silaha haijawahi kutumika popote duniani, Rais Donald Trump alitaka kuishambulia North Korea ambapo vita hivyo vingeleta madhara makubwa sana kwani Northe Korea wangeshambulia South Korea na Japan kwa silaha za maangamizi na mamilioni ya watu wangeuawa.
Dr James Gilligan professor kutoka New York University aliambia kikao akiwa kama daktari bingwa wa akili na uzoefu wa kugundua mtu mwenye matatizo ya akili kwa kipindi kifupi Rais Donald Trump yupo madarakani amegundua mapungufu makubwa ya kiakili ya Donald Trump.
source: Presstv.
 
wapuuzi hao wanamkosea heshima kiongozi wa nchi
hawajui kwa kusema hivyo wamewatukana watu waliomchagua au wanadhani amejieka

 
Wajinga sana, kama wameshindwa kugundua upungufu wa akili za Mapanki? Kweli wehu, unajua ukiwa Dr wa vichaa shurti na wewe uwe kichaa, sishangai hao vichaa waliokusanyika. Bali nashanga hicho chuo walichofanyia mkusanyiko wao.
 
Ukimwona kichaa ameshika panga unatakiwa utumie akili sio nguvu kumpokonya hiyo silaha ili asikudhuru wewe au yeye mwenyewe.
Rais Donald Trump anataka kutumia nguvu za kijeshi kuzuia Korea Kaskazini asiwe na silaha ya nuklia wakati Rais wa Korea ni Chizii anaweza kutumia silaha za maangamizi dhidi ya majirani zake,
Huo ni mfano tosha Donald Trump naye ni chizi.
 
Ule uchaguzi safari hii umeacha mgawanyiko na mpasuko mkubwa sana kiasi wakiendelea kama hivi wataishia kubaya hawa, na kwa hali hii bado wanataka kuvamia mataifa ya watu kweli?
Sasa si yatakuwa kama yaleyale ya kuwakimbia Vietcong maji yalipofika kwa shingo!
Yani unaanzaje kwenda vitani ukiwa kwenye hali ya mgawanyiko na mvurugano kama hivi.
 
Back
Top Bottom