Habari wanajukwaa,
Kuna hili suala la usajili wa wataalamu wa maabara Tanzania, hili ni jambo zuri ili kupata wataalam waliokidhi vigezo vya kutoa huduma.
Nina tatizo juu ya utaratibu unaotumika, wao husajili mtu kwa kumpa hati ya muda(provisional registration) ambayo huitumia kwa miezi kumi na mbili baada ya hapo huhitajika kufanya mtihani ili aweze kupata usajili kamili.
Ikumbukwe huyu mtu anakuwa ameshamaliza mitihani ya mwisho na kuifaulu kwa viwango vilovyowekwa na baraza.
Swali: Kuna ulazima gani wa kufanya mtihani baada ya mwaka mzima wa kuhitimu moduli zako zote ulizofaulu?
Maoni: Wizara iweke utaratibu wa kufanya mtihani huo pindi muhitimu anapokuwa anafanya mtihani wake wa mwisho ili kuondoa usumbufu wa kufanya mitihani mara mbili mbili kana kwamba wizara haziaminiani.