Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Mwaka 1985, Mwalimu Julius Nyerere (marehemu), akiwa na umri wa miaka 63, aling'atuka nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi (Urais), kipindi hicho, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilikuwa inamruhusu kuendelea kukitetea kiti chake, vilevile hakuwa na mpinzani yeyote wa kisiasa.
Stephen Masato Wasira, mwenye umri wa miaka 70, ameshinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwania Ubunge wa Bunda Mjini kwa muhula mwingine wa miaka mitano.
Mwaka 1990, Mwalimu Nyerere akiwa na umri wa miaka 68, akiwa na afya njema kabisa, alikabidhi mamlaka ya uongozi wa CCM (uenyekiti) kwa Rais wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Wasira, anataka amalize ubunge akiwa na miaka 75, na si ajabu akataka kugombea tena baada ya hapo.
Mwalimu Nyerere alipokuwa anaachia ngazi alitoa sababu kadhaa, mojawapo ikiwa kuwaachia vijana wenye mawazo mapya waongoze nchi, pili alisema anataka awe pembeni ili abaki kuwa mshauri na mwelekezi wa vijana, tatu alieleza kuwa ni heshima kuachia madaraka kipindi bado anapendwa, kwani mtu anapoongoza kwa muda mrefu huwachosha wananchi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ana umri wa miaka 67 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, umri wake ni miaka 63. Wote hao wametangaza kuwa hawatagombea tena ubunge baada ya vipindi vyao vitatu. Wasira aliyeanza kula keki ya taifa tangu utawala wa Mwalimu Nyerere ukiwa mbichi kabisa, anataka kuendelea!
Wakati wastani wa kuishi kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida hauzidi miaka 60, Wasira anataka aendelee kuwa mbunge, katika umri ambao ameshavuka kiwango cha kawaida cha kuishi.
Sensa ya mwaka 2012, ilikuja na majibu kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wapo chini ya umri wa miaka 35. Na wale wenye kuzidi umri wa miaka 70, hawatimizi hata asilimia moja. Wasira aliye kwenye kundi dogo mno, anataka awe mbunge. Yaani aliye ndani ya asilimia moja, aende kuwasemea watu zaidi ya asilimia 80.
Kundi hilo kubwa, Wasira alilivuka takriban miaka 40 iliyopita. Zaidi, mahitaji ya vijana wa zama zake si wa sasa. Yapo mabadiliko makubwa ambayo yanahitaji fikra zinazonyumbulika kulingana na wakati wa sasa. Wasira mbele ya Watanzania walio wengi ni sawa na wajukuu wa wajukuu zake. Hapo hakutakuwa na uwiano wa uwakilishi.
Maandiko matakatifu yanaeleza mgawanyo wa maisha, kwamba kwa kawaida mtu anaishi makumi manne moja (yaani miaka 40), na mwenye afya imara kwelikweli anaweza kujitahidi mpaka kufikisha makumi manne mawili (miaka 80), baada ya hapo ni matatizo. Ni maradhi yasiyokwisha, kupoteza kumbukumbu, kuanikwa juani na kadhia nyingine chungu tele.
Kutokana na tafsiri ya maandiko matakatifu kuwa kiwango cha juu cha kuishi ni miaka 80, na kwa vile Wasira akifanikiwa kuwa Mbunge wa Bunda Mjini kwa kipindi kingine cha miaka mitano, na Mungu akimuweka hai atamaliza akiwa na miaka 75, ni sawa na kusema anataka kuwa mbunge mpaka umri wake wa mwisho. Huu ni ubinafsi uliopitiliza.
Ni kama Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe. Anataka nafsi iache mwili akiwa Ikulu. Na Mungu anaamua kumwacha aendelee kuvuta pumzi ya uhai. Matokeo yake inakuwa aibu kila siku, mara aanguke jukwaani, wakati mwingine kwenye zulia jekundu mbele ya kadamnasi. Mara asinzie kwenye mikutano ya Kimataifa, na kupoteza kumbukumbu. Hayo ndiyo yamekuwa sehemu ya maisha yake.
Wasira si kwamba hajui kuwa ameshachoka, ila ndiyo ile methali "Yuajifanya chongo angaona." Kwamba anajifanya chongo lakini anaona. Anajua kabisa ni yeye aliyetawala vyombo vya habari na picha zake akiuchapa usingizi bungeni. Anapaswa kujiuliza mwenyewe, je, udhaifu alionao leo, unalingana na afya aliyokuwa nayo miaka 25 iliyopita?
Umakini wake wa sasa, unashabihiana na ule aliokuwa nao kipindi anateuliwa na Mwalimu Nyerere? Je, yeye anapingana na kauli ya Baba wa Taifa kwamba kuongoza kwa muda mrefu ni kuwachusha wananchi? Umahiri alionao leo wa kupambana kisiasa, unalingana na ule wa mwaka 1995, alipohamia NCCR-Mageuzi?
Jibu lipo wazi, yeye, mimi na wewe, wote kwa pamoja tunalijua. Vilevile, watu wote ambao ndiyo kizazi chake cha kisiasa, tayari walishaweka daruga pembeni na kupisha mawazo mapya, yeye ameendelea kung'ang'ania. Ananitisha, amenifanya nihofu kuwa kama ingetokea angekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, angeweza kupindisha hata katiba ili abaki madarakani.
Ni mchoyo wa kupokezana na wengine! Fikiria kuwa Samuel Sitta alitangaza tangu baada ya Uchaguzi Mkuu 2010 kuwa akimaliza miaka yake mitano, hatagombea tena ubunge na kweli ametekeleza hivyo. Sitta ni umri unaokaribiana na Wasira ambaye msamiati wa kustaafu haupo kabisa ndani ya kichwa chake.
Maveterani wengine wa kisiasa, Paul Kimiti, Crisant Majiyatanga Mzindakaya na wengineo, kwa hiari yao, walitangaza kuachana na siasa wakiwa chini ya umri wa miaka 70. Ukimwambia Wasira aige mfano huo, anaweza kukunasa makofi. Kumbuka, aliwahi kumpa kichapo mwandishi wa habari miaka ya 1990 alipokuwa NCCR-Mageuzi.
Jambo moja tu la kujiuliza; Wasira yupo kwenye ulingo wa siasa katika ngazi ya uteule wa Rais kabla hata ya Rais Jakaya Kikwete. Leo hii JK anasubiri miezi ili ampishe Ikulu Rais wa Awamu ya Tano, wakati Wasira ndiyo kwanza yupo kwenye mbio za kuusaka muhula mpya wa miaka mitano. Zingatia kuwa Rais Kikwete ana miaka 65 tu.
Wasira ni mteule wa Rais tangu mwaka 1965, yaani miaka 50 iliyopita. Ni mbunge tangu miaka 45 iliyopita, kwani mwaka 1970, alichaguliwa kuliongoza Jimbo la Mwibara, baadaye Bunda. Amekuwa ndani ya Baraza la Mawaziri tangu miaka 42 iliyopita. Hii ni zaidi ya ajira ya kudumu, hii ni ajira ya maisha!
Ongezea kuwa alipata bahati ya kuwa mteule wa kitaifa tangu akiwa na umri wa miaka 20 tu. Na alishinda ubunge akiwa na umri wa miaka 25 tu na ni waziri tangu akiwa na umri wa miaka 28 tu, sasa ana miaka 70, yupo tu na anahitaji kuendelea kuwepo. Maisha yanataka nini kwake?
Rais Kikwete alianza kuitumikia Serikali Kuu mwaka 1988 na alikuwa mbunge kuanzia mwaka 1990. Hapo jumlisha na miaka 10 ya Urais, anakwenda kustaafu. Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Tluway Sumaye, alikuwa Mbunge wa Hanang kwa miaka 15 tu, na baada ya hapo aliamua kujiweka pembeni. Huu ndiyo uungwana!
Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji, hivi karibuni aliitisha mkutano wa hadhara jimboni kwake na kuahidi kuwa hatagombea tena baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa August 26, mwaka huu. Alisema miaka 10 aliyowatumikia imekuwa ni heshima kubwa kwake lakini inatosha, kwa hiyo anapisha mawazo mapya kwa ajili ya kulipeleka mbele zaidi jimbo hilo.
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, naye alifanya uamuzi wa kuhama jimbo la Kigoma Kaskazini baada ya kuliongoza kwa miaka 10. Hoja ya Zitto ni kuwa miaka 10 ilitosha, kwani kama kuna vitu alishindwa kuvifanyia kazi, ihesabike ni changamoto zilizomshinda. Vilevile Zitto amekuwa muumini wa kuwepo ukomo wa vipindi vya ubunge, mathalan miaka 10 kisha mbunge anastaafu.
Ukiachana na hilo la ulinganifu na watu wengine, kuna swali ambalo mimi na wewe tunapaswa kujiuliza, kadhalika hata yeye mwenyewe Wasira. Je, kwa miaka 50 ambayo amekuwa kiongozi na miaka 45 ya ubunge, ni nini ambacho amekisahau, mpaka ang'ang'anie ubunge kwa miaka mingine mitano?
Si ajabu akishinda, atataka agombee tena mpaka mwaka 2025. Wakati huo atakuwa na umri wa miaka 80. Sina uhakika kama hapo atatosheka au atahitaji kuendelea. Hapa ndipo Napata picha kuwa ndiyo maana mwaka 1995 aliposhindwa kura za maoni na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, aliamua kuwa Msambaa na kusema "Kama Mbwai Mbwai", huyo akaenda NCCR-Mageuzi na kushinda ubunge. Akaendelea kuula!
Kama atashinda ubunge na Rais ajaye kuamua kumtumia kwenye Baraza la Mawaziri kwa kipindi kingine, maana yake anaweza kuwa waziri kwa hata miaka 52, Wasira hachoki! Hasemi lakini ndani ya kichwa chake, anaamini yeye peke yake ndiye mwenye mawazo mazuri kuwawakilisha wananchi bungeni na kutumika wizarani, hakuna mwingine anayetosha kumkabidhi kijiti.
Kwa kifupi ni kwamba Wasira amechoka, labda anachohofikiria ni baada ya kuachana na ubunge ni nini kingine atafanya. Uvaaji wa "Wasira Style", yaani ule mtindo wa kuvaa koti kwa kupishanisha vifungo, mpaka kumfanya afanane na mganga wa kienyeji, inathibisha kuwa mzee wetu siyo yule tena wa miaka hiyo.
Uchovu unaochangiwa na uzee pamoja na utumishi wa muda mrefu, umemfanya wakati mwingine apoteze umakini wa kuvaa. Kifungo cha chini anakifunga juu au cha juu anakifunga chini kisha anatoka hivyohivyo kwenda kwenye majukumu ya kitaifa. Kama hili halioni kuwa ni kipimo tosha kuwa amechoka, basi mzee wetu ni king'ang'anizi sana.
Jumlisha na ile hali ya kusinzia bungeni, kwa hakika anapaswa kuachia wengine, hususan vijana ili nao wathibitishe karama zao. Kuendelea kugombea, kwanza ni ubinafsi kujiona ni yeye pekee anastahili, pili ni kuwanyima wananchi haki ya kuwa na kiongozi anayeendana na matakwa ya wakati uliopo, tatu ni kuwanyima fursa watu wengine wenye uwezo.
Zaidi, kama atagombea na kushinda, makosa yatakuwa ya wananchi wenyewe kushindwa kumkataa kiongozi anayelala bungeni, aliyechoka mpaka kupoteza umakini, hivyo kuvaa makoti hovyohovyo.
Majukumu yanachosha kama unawatumikia wananchi kwa wito, Rais Kikwete alisema, miaka 10 ya Urais hatamani kuongeza hata mwaka mwingine mmoja. Uking'ang'anizi wa Wasira unanifanya nione hana wito, isipokuwa anatumikia ajira!
Alikaribishwa na Mwalimu Nyerere ambaye aliondoka na kumwacha. Akaendelea kung'ara vilivyo chini ya Rais wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin William Mkapa alikuwa mbunge wa upinzani kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Awamu ya Nne amekuwa mbunge CCM na waziri kipindi chote cha miaka 10, bado anataka Rais Kikwete aondoke, yeye abakie.
Tafadhali sana Wasira!
By Luqman Maloto. (Imetoka Jambo Leo)