Wasomi wetu ni vituko sana hakika

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,710
Reaction score
4,046
Wakati huu kuna mkutano wa maendeleo ya miundo mbinu ktk jiji la dar kati ya mkuu wa mkoa, madiwani, wenyeviti wa mitaa na mainjinia wa jiji.

Vituko vimeanza mara baada ya mkuu wa mkoa kuruhusu mainjinia na wasomi na wasimamizi wa miradi mbali mbali ya jiji, wasomi Hawa wamegeuka wachekeshaji wakubwa kwa kushindwa kwao kujielezea ata kidogo kuhusu kile wanachokifahamu toka ktk miradi wanayoisimamia.

Mkurugenzi mzima wa Tanroads wilaya anasema tatizo la kuaribika kwa barabara ya Mwananyamala hospitali kua pale kuna tatizo sana la mvua, mvua inaharibu ile barabara, injinia mzima anaitwa ajieleze aseme kwanini barabara hazitengenezwi na pesa zinatolewa, anasema eti yeye ni mgeni pale halimashauri, anaulizwa ana muda gani tangia ahamie pale halmashauri anadai ana miaka miwili tu bado mgeni sana.

Sasa boss mzima msomi kabisa na anaongoza dawasco anasema tatizo la wananchi hawafikishi malalamiko yao dawasco kwa njia ya dawasco app. ' tena hatoi ata ufafanuzi app ni kitu gani na je kila mwananchi hapa nchini ana smartphone? Anaulizwa zaidi anasema yes ofcoz ilo tatizo wananchi wanawapigia wrong managers.

Kwa kweli wasomi hawa wako zaidi ya 30 hapa na wanajibu kwa aina moja ya ujibuji wao, na hata hawa tusiwalaumu njoo mitaa na makazini hali ni hii hii.

Tuishie hapa tu, tusije tukatukanwa mengi matusi.
 
mi sijui kwanza mie ni mgeni maeneo hayo....fukuzaa wapigaji hao watumbuliwe tu maana hakuna namna.
 
Ndio tatizo la kukariri Mkuu.

Wasomi wengi hawajui kujieleza, kuelezea Jambo Kwa ufasaha likaeleweka.

Wasomi wengi uwezo wao wa kufikiri upo chini hasa kuhusu ishu za maendeleo. Ndio maana kuna tofauti ndogo Kati ya mtu aliyesoma na Yule asiyesoma Kwa kizazi cha kuanzia miaka ya 90.

Wasomi wengi hawapendi kusoma wala kujifunza Kwa undani mambo yaliyo katika Kada zao mara baada ya kuhitimu. Hii pia ni changamoto.

Unaweza kuta Msomi Fulani ni Daktari lakini uwezo wake ni mdogo kuanzia mitindo ya maisha hadi mienendo na tabia.

Mtu ni Mwalimu lakini Akili zake hazina tofauti na Wanamuziki wasio enda shule. Kuanzia uvaaji mpaka muonekano. Nae ni Msomi.

Wasomi wengi Akili zao ni ki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda Angepewa Awe Mkuu Wa Mkoa Wa Pwan ,bagamoyo Na Dar Yan Asingeteteleka Walah. Yan Msomi Mzima Anaulizwa Anasema Tatizo Ni Mvua Wenzetu China Wamejenga Wagolofa Yenye Springi Kwenye Maeneo Yenye Tetemeko Sasa Sisi Eti Mvua Tu Ndo Ttz
 
Wewe ukiwa mmoja wapo ( ndan ya wasomi)

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 


Mkuu nimekuelewa sanaa, na tena hapo kwenye life styles ndio kuna utata unakutana na kijana ni lawyer au injinia lakini kanyoa kiduku au kavaa nguo za kubana sanaa
 
Lipumba na Chenge ndo wasomi nao waelewa sana maana wanatuonyesha elimu ni nn[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 

Naamini Chata ni Msomi mzuri tu, naomba nikukumbushe tu sikukosoi Mkuu
kuharibika
Halimashauri
 
Sasa inabidi tupambane na wasomi uchwara wasiojielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…