Wasomi wa Tanzania na rushwa

Wasomi wa Tanzania na rushwa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,277
Reaction score
13,920
Tanzania ya sasa inasikitisha maana badala ya kujivunia wasomi wetu tumebakia na aibu na majanga yanayoletwa na wasomi wetu kwa rushwa.

1. Chenge: Chenge ni kati ya wasomi wa hali ya juu Tanzania kwa ukweli kuwa kasoma Harvard ambayo ni chuo na kina shika namba moja duniani kwa umahiri na historia. Havard ni kati ya vyuo vikuu vya kwanza kuanzishwa kwenye dunia hii. Lakini badala ya kusaidia nchi Chenge amekuwa akitumia elimu yake kujinufaisha binafsi. Hata kwenye swala la katiba alihakikisha anashikilia na kuzuia mambo yote ambayo ni ya kuhusu rushwa.
2. Prof Tibaijuka: Huyu mama ni kati ya wasomi mahiri Tanzania na mwenye uzoefu wa hali ya juu lakini amebakia kuibia nchi ambayo imempa jina na kumsomesha.
3. Prof Muhongo: Kama mama tibaijuka ni aibu tu katuletea badala ya kusaidia nchi

Mimi mawazo yangu ni kwamba badala ya kuangalia usomi Tanzania ingekuwa mbali kama ingekuwa inaajiri watu wanaojua kutawala na kutatua matatizo. Kuna wafanya biashara wa maduka ambao wangeweza kutuletea mikakati ya maendeleo kuliko hawa wasomi ambao ni hasara na janga la taifa. Usomi pekee haotoshi tuwe na utamaduni wa kuangalia utendaji. Utamaduni wa ma Prof, Dr kuingia kwenye siasa na kudanganya watu kuwa wanajua zaidi hauna ukweli hasa kimaendeleo! tutatufe Watanzania wenye vipaji vya kuleta maendeleo badala ya kudanganyika na elimu za watu!. Kuwa Prof au Dr haina msingi wowote wa wewe kuwa kiongozi mzuri kwasababu hizo research za kuwa Dr si za utawala na si mafunzo ya kutawala!
 
Sidhani kama usomi ni kigezo cha kuwa kiongozi bora.Tanzania tuna viongozi bora ambao ni elimu ya ngumbaro.Lakini pia nitanabahishe kuwa wasomi wachache wanaipaka matope nchi yetu kwa ulafi binafsi na hulka ya wizi huku wakitumia mipenyo dhaifu iliyopo.Tukumbuke tulikuwa na mtu kama Dr.Tuntemeke Sanga,msomi lakini alikuwa na uchungu na nchi yake na mpaka anakufa alikuwa mtu wa kawaida sana.Tulikuwa na watu wasiokuwa wasomi lakini viongozi bora kama akina Kuwayawaya S.Kuwayawaya (Mb) na waliitumikia nchi kwa namna ya pekee sana na hawakuwa na tamaa hata kidogo.Kwa hiyo ulafi,wizi na hulka ya udanganyifu ni tabia tu ya mtu binafsi na kamwe hainakisi usomi au u-ngumbaro wa mtu.
 
Back
Top Bottom