Waso asili na Kiswahili wakipenda sana kuliko sisi waswahili?

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,827
1,729
Congo wajivunia sana Kiswahili , Kinshasa ukiwa mswahili wathaminiwa hasa, na utapata marafiki wengi tu. Uganda wakitamani lakini kinawagonga kweli weli na ukikiongea hukosi mwali.

Wenzetu wakenya wanalijua hili na ukikutana na Mkenya Nje ya East Africa hata ona haya kuongea nawe kiswahili tofauti na waswahili sisi.

Wacha niseme tu ukweli potelea mbali mkinisema kwamba najitapa. Nimefika Kinshasa nikasali Masjidi Gombe , japo mawaidha yalikua ya French na Lingala ila huko nje nilipata fursa ya kuonana na waswahili wa Kisangani na hapo tulikimwaga hasa.

Conte d'ivore kule nilikuta na Wakenya wakifanya kazi UN, hawa ndio kabisa wenyewe nje ya nchi ya ni waswahili kabisa na hawaoni haya.

South Sudan , wanaongea kiswahili pale soko la Konyokonyo wanganda na wakenya kiswahili tu.

Sasa shida ukutane na masanja kule NYC mama weeee utadhani hatoki Bunju.
 
Yes! Ahm! Yeah I know kiswahili in small zan kingereza I am English!!! (Hapo umukutana na Harmonize Houston USA akipiga show zake za kigodoro)
 
Back
Top Bottom