Wasiojua wanapojaribu kuweka zuio la sala

Let Love Reign

JF-Expert Member
Apr 24, 2018
613
364
KWA KADRI YA WALIVYOZIDI KUWAZUIA KUSALI NDIVYO WALIVYOPAZA SAUTI ZAO!
===================================
KWA KADRI YA WALIVYOZIDI KUWATESA NDIVYO WALIVYOZIDI KUONGEZEKA NA KUZIDI KUENEA!
==============

WATU WA IMANI TUNAPOKUTANIKA KUSALI KWA JINA LA YESU, TUNAO USHUHUDA, TUNAJUA HUYU MUNGU WETU ALIVYOTUTETEA, ALIVYOTUPONYA, NA KUTUPATIA AMANI MIOYONI MWETU;

Maana tumeagizwa kuwa;
(Wala tusiache kukusanyika pamoja(KUSALI), kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. EBR. 10:25

TUNALO TUMAINI TUKIKUMBUKA KUWA;
Farao mtoto akiwa kama kiongozi wa taifa la Misri, aliazimia kuwazidishia utesi watu wa imani, Wayahudi, walipokuwa Misri.
Pengine hakujua Historia ya baba zake waliomtangulia KATIKA UONGOZI kuwa kupitia SALA za mtu wa Mungu Yusufu, Mungu akaliokoa Taifa la Misri na njaa ya miaka saba, iliyolenga kulimaliza taifa la Misri.
FARAO Mkubwa, kama kiongozi wa taifa la kipagani, alitambua, UNYETI WA SALA NA HEKIMA YA WATU WA IMANI ndip (Farao akawaambia watumwa wake, TUPATE WAPI MTU KAMA HUYU, mwenye roho ya Mungu ndani yake? MWANZO. 41:38
Hii inadhihirisha unyeti wa watumishi wa Mungu, na watu walioshika imani kufanya sala kwa Mungu, hata kumfanya Farao, kuuliza je kuna mtu kama huyu ambaye Roho wa Mungu(ROHO MTAKATIFU) yupo ndani yake?

Lakini Farao mdogo, hakujua hili, kama ilivyo kwa wengi, kwa udanganyifu wa elimu zao za kidunia, ama nafasi walizozipata, hudhani wao wajua zaidi kuliko wazazi wao waliowatangulia na hivyo kwa agizo lake Farao. ...(wakaweka wasimamizi juu yao WAWATESE kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. LAKINI KWA KADRI YA WALIVYOWATESA NDIVYO WALIVYOONGEZEKA na KUZIDI KUENEA. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.KUTOKA. 1:11‭-‬12)

Ndivyo ilivyokuwa wakati Dario akiwa kiongozi wa Taifa kubwa la Babeli, kwa ushawishi wa baadhi ya viongozi wa kipagani, AKAWEKA SHARTI LA WATU KUTOSALI SAWA NA IMANI, ISIPOKUWA KWA AGIZO LAKE.

LAKINI HAKUJUA KUWA WOKOVU WA TAIFA HILO, ULIKUWA MIKONONI MWA WATU WA IMANI!, Kina Daniel, Meshaki, Shadraki na Abednego, watu wa imani, waliokuwa wakisali mara tatu kwa siku, kila siku.
Lakini kwa wapagani wa babeli, Sala za kina Danieli kila mara waliposali, ziliharibu malengo yao, na hivyo kuja na mpango wa kuvuruga sala za kina Danieli.

Lakini, (Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) AKAPIGA MAGOTI MARA TATU KILA SIKU, AKASALI, AKASHUKURU MBELE ZA MUNGU WAKE, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
DAN. 6:10)

Na walipomkamata Daniel, KWA SABABU YA KUSALI KWAKE, NA KUMTUPA KWENYE TUNDU LA SIMBA, NDIVYO ALIVYOZIDI KUSALI,naye MUNGU akamuokoa na Simba wakali, na hata kulipokucha, mfalme akaja kumtazama Daniel ajue kama ameuawa au la maana alijua kuwa Agizo lile halikuwa jema bali lililenga kuwazuia watu wa imani WASISALI, na (Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele. Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.DANIEL. 6:21‭-‬22)

Lakini watesi wake waliomzuia KUSALI Mara tatu kwa siku kwa kuelekeza uso wake Yerusalem wakaishia wao kuingizwa tunduni, na kuliwa na Simba.

Mungu wetu ameagiza akisema;
(ombeni (Salini) bila kukoma; 1 THE. 5:17)

Wanaposimama kusali, si tu wanalilia shida zao pekee, bali huombea neema, rehema na amani ili maovu yasitokee juu yao na juu ya nchi maana ni agizo la Mungu akisema;
(Ila ombeni yasitokee hayo.... MK. 13:18)

Lakini pia ni muhimu kinua kiwa furaha yetu haitimiliki kwa kuwa na mali, ama pesa tu, isipokuwa kila tunaposali tukijua kuwa ni njia ya kuwa na ushirika wa karibu na Mungu wetu, maana Bwana wetu Yesu aliagiza akisema;
( Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. YN. 16:24)

Mitume wake Bwana Yesu, WALIPOZUIWA KUSALI na kukusanyika kumhubiri Yesu, ndivyo walivyozidi KUSALI, huku wakimtumikia Mungu, na hata walipokamatwa kwa kusali na kuhubiri, wakikemewa na kuonywa kutosali na kulitaja jina la Yesu, wakiongozwa na Roho mtakatifu; Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba JE NI HAKI MBELE ZA MUNGU KUWASIKILIZA NINYI (wanadamu) KULIKO MUNGU, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
MDO 4:19‭-‬20

Lakini pia ijulikane kuwa tunapokusanyika KUSALI kila mara, tunakutana tukishuhudiwa nafsini mwetu kuwa;
(BWANA ASIPOIJENGA NYUMBA WAIJENGAO WAFANYA KAZI BURE. BWANA ASIPOULINDA MJI YEYE AULINDAYE AKESHA BURE. Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.ZAB. 127:1‭-‬2 )

TUNAPOKUTANIKA KUSALI, TUNATIMIZA AGIZO LA MUNGU, NA KUSUDI LA MUNGU kama ilivyoandikwa;

(Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa BWANA.
ZAB. 122:1)


Source:pastor Stanford Chijenga(facebook)
 
Wanataka kujenga nchi ya Wapagani,watu wasiokuwa na hofu ya Mungu ndani yao, Mumiani na watoa roho za watu. Ili kulifanikisha hili lazima waweke kanuni zitakazowazuia raia wema, kukaa na kutafakari juu ya Mungu wetu. Nasema, WASITUTISHEEEEE( In Maalim Seif's voice).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom