SECRET AGENT
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 254
- 499
OkAli Bongo Ondimba alizaliwa Februari 9 mwaka 1959 mjini Brazzaville na alifahamika kama mwana wa Alain Bernard Bongo (baadae Omar Bongo Ondimba) na Josephin (baadae Patience Dabany).
Kumekuwa na mjadala ikiwa Ali Bongo ni mwana wa Omar Bongo ikizingatiwa kuwa mama yake alikuwa mja mzito miezi 18 kabla ya kuolewa madai ambayo Ali Bongo amekuwa akipinga.
Baada ya kusomea uwanasheria Ali Bongo alijitosa katika siasa za Gabon ambapo alijiunga na chama PDG mwaka 1981 na muda mfupi baadae aliteuliwa katika kamati kuu ya chama mwezi Machi mwaka 1983.
Baadae aliteuliwa kumwakilisha baba yake katika chama hicho nafasi ambayo ilimwezesha kujiunga na asasi kuu ya uongozi wa chama katika uamuzi ambao ulifikiwa katika kongamano maalum ya PDG mwaka 1986.
Ali Bongo ni mwana wa kiume wa rais Omar Bongo, ambaye aliongoza Gabon kiimla kutoka mwaka 1967 hadi alipofariki dunia mwaka 2009.
Wakati wa utawala wa baba yake Ali Bongo aliwahi kuhudumu kama waziri wa mambo ya nje wa wa Gabon kati ya mwaka 1989 na 1991.
Pia aliwahi kuhudumu kama naibu kiongozi wa bunge la kitaifa kuanzia mwaka 1991 hadi 1999.
Wakati wa uchaguzi wa uraisi wa mwaka 2005 alifanya kazi kama mshirikishi wa vijana katika kampaini ya baba yake.
Baada ya uchaguzi huo alipandishwa cheo na kuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Gabon kuanzia Januari 21 mwaka 2006 huku akiendelea kushikilia wadhifa wa waziri wa ulinzi.
Alishikilia wadhifa huo hadi mwaka 2009.
Ali Bongo alitarajiwa kuwa mrithi wa baba yake Omar Bongo ikizingatiwa kuwa alimteua katika nyadhifa muhimu katika utawala wake.
Hata hivyo uungwaji mkono wa Ali Bongo ndani ya uongozi wa chama cha PDG ulihojiwa na vyombo vya habari na kulikuwa na maoni kwamba raia wengi wa Gabon walimchukulia kama ''mtoto aliyedekezwa na kwamba hawezi kuwasiliana kwa lugha asilia ya nyumbani kwasababu alizaliwa Congo-Brazzaville, kulelewa nchini Ufaransa.
Kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa madarakani kwa miaka 41, alichaguliwa kuendelea na uongozi wa taifa hilo mwezi Agosti mwaka 2009.
Siku chache baada ya uchaguzi uliyofanyika Agosti 30 mwaka 2009 alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata 42% ya kura.
Matokeo ya uchaguzi huo yaliidhinishwa mara moja na mahakama ya kikatiba.
Upinzani ulipinga matokeo hayo rasmi ya uchaguzi ukidai kuwa ulikumbwa na udanganyifu.
Hatua ambayo ilisababisha maandamano makubwa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Gabon.
Ili kujibu madai hayo mahakama ya katiba iliamuru kuwa kura za uchaguzi wa uraisi zihesabiwe upya.
Ali Bongo aliibuka tena mshindi baada ya kupata 41.79% ya kura zote zilizopigwa wakati wa uchaguzi uliyofanyika oktoba 12 mwaka 2009.
Aliapishwa kuwa raisi wa Gabon oktoba 16 katika hafla iliyohudhuriwa na marais kadhaa wa mataifa ya Afrika.
Rais Ali Bongo ana mke na watoto wanne.
SOURCE: BBC SWAHILIView attachment 989098
Sent using Jamii Forums mobile app
Hajapinduliwa jaribio la kupindua lilishindikana..Asante kwa tàarifa yako nusu,maana hujasema kama kapinduliwa na sasa nchi iko chini ya jeshi
Sent using Jamii Forums mobile app
Baba yake ndio utakuwa umemsikia sanaHuyu mtu nimemsikia sana
Fuatilia thread zangu za cku za nyuma , ipo ya kuhusu jaribio la mapinduzi na ipo ya serikali kulizima jaribio hiloAsante kwa tàarifa yako nusu,maana hujasema kama kapinduliwa na sasa nchi iko chini ya jeshi
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu taarifa yako iko sahihiHajapinduliwa jaribio la kupindua lilishindikana..
Sawa mkuu nakuelewa sanaFuatilia thread zangu za cku za nyuma , ipo ya kuhusu jaribio la mapinduzi na ipo ya serikali kulizima jaribio hilo
Sent using Jamii Forums mobile app
Ali Bongo Ondimba alizaliwa Februari 9 mwaka 1959 mjini Brazzaville na alifahamika kama mwana wa Alain Bernard Bongo (baadae Omar Bongo Ondimba) na Josephin (baadae Patience Dabany).